Corona: Kitakasa mikono hiki hakina madhara ya kiafya

February 2, 2021 7:38 am · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni kitakasa mikono aina ya Farah ambacho kimezushiwa kuwa kinaleta madhara kwenye mikono wakati wakukitumia.
  • Hakuna ripoti yoyote iliyotolewa inayoonesha bidhaa hiyo inaleta madhara ya kuvimba mikono.

Dar es Salaam. Moja ya tahadhari inayoshauriwa na wataalamu wa afya ili kujinga na ugonjwa virusi vya Corona ni kutumia vitakasa mikono mara kwa mara. 

Lakini baadhi ya watu wanadai kuwa zinasababisha madhara kwenye viganja vya mikono ikiwemo kuvimba na kujaa maji. Hata hivyo, hakuna taarifa rasmi iliyotolewa na mamlaka za afya duniani kuhusu madhara yatokanayo na matumizi ya vitakasa mikono.

Miongoni mwa habari hizo za uzushi kuhusu vitakasa mikono zinazosambaa mtandaoni ni ile inayowataka watu waache kutumia kitakasa mikono aina ya Farah kinachotengenezwa na kampuni ya The National Detergent Company ya nchini Oman. 

Habari hiyo ambayo imeambatana na  picha mbili za mkono wa mtu aliyevimba na kitakasa mikono cha Farah inawataka watu wasinunue kwa sababu ina madhara. Kimsingi habari hiyo ni uzushi na haina ukweli wowote.


Ukweli uko wapi?

Hata baada ya timu ya Nukta Fakti kwa kutumia zana ya kidijitali ya Google Reverse Image kubaini ukweli wa picha hiyo ya mkono wa mtu uliojaa maji, hatukufanikiwa kuipata na haina uhusiano na matumizi ya vitakasa mikono. 

Pia kitasa mikono aina ya Farah bado kinatumika na hakuna mahali popote kilipopigwa marufuku kwa sababu kimekidhi vigezo vinavyohitajika sokoni. Hata Wizara ya Afya ya Oman imekithibitisha kitakasa mikono hicho na kupendekezwa kutumiwa na watu. 

“Bidhaa hii imetengenezwa katika viwango vinavyotakiwa na kusaidia katika kujikinga na maambukizi ya Corona,” inaeleza sehemu ya maelezo ya bidhaa hiyo inayotumika katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo Farme za Kiarabu (UAE) na Qatar. 


Zinazohusiana:


Nalo Shirika la Afya Duniani (WHO) ambalo lina dhamana ya kulinda afya za watu halijatoa tamko lolote kuhusu madhara ambayo watu wanaweza kuyapata wakati wa kutumia vitakasa mikono, licha ya kuwahimiza watu kutumia bidhaa hiyo kama njia mojawapo ya kujikinga na Corona.

Hata hivyo, WHO inasisitiza zaidi watu kunawa mikono kwa maji tiririka mara kwa mara kwa sababu ni nji rahisi ya kujikinga na ugonjwa huo. 

Njia nyingine za kujikinga ni pamoja na kuvaa barakoa, kupiga chafya au kukohoa kwa kutumia tishu na kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima.  

/
No matches found for this filter
31 May, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
31 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
31 May, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

Nukta TV

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

Nukta TV

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

Nukta TV