Vifaa vya vitakasa mikono havienezi Uviko-19
- WHO yasema mtu akipata kitakasa mikono anajiweka salama.
- Yasisitiza watu kuendelea kutumia.
Dar es Salaam. Huenda umesikia au na wewe ni mmoja wa watu wanaogopa kugusa chupa au vifaa vyenye vitakasa mikono (sanitizers) katika maeneo ya umma kwa madai kuwa vinasambaza virusi vya Uviko-19, fahamu kuwa umedanganywa.
Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema vifaa hivyo ni afua muhimu ya kujikinga na ugonjwa huo hasa katika maeneo ya umma ambayo watu hulazimika kushika vitu kama milango.
WHO inasema ikiwa mtu amepaka kitaka mikono tayari unakuwa salama, hata akishika kifaa cha afua hiyo hawezi kupata virusi kwa sababu mikono yake imekuwa imetakaswa.
“Ikiwa mtu atatumia kitakasa mikono kwenye mikusanyiko ya watu, hatari ya kupata wadudu ni ndogo na atasaidia kuwawezeka watu wengine salama,” imeeleza WHO katika ufanunuzi wake kuhusu uzushi huo.
Ili kujikinga na ugonjwa huo ambao bado unaitesa dunia, wanshauriwa kupata chanjo na kuendelea kutumia vitakasa mikono, kuvaa barakoa, kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima na kunawa mikono kwa maji tiririka.