Ghana yawa nchi ya kwanza kupokea chanjo ya COVID-19 chini ya programu ya Covax

February 25, 2021 6:46 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Shehena ya kwanza ya chanjo aina ya AstraZeneca / Oxford zilizotolewa COVAX imewasili nchini humo jana Februari 24, 2020.
  • Programu hiyo maalum ya COVAX inayosimamiwa na Umoja wa Mataifa (UN) inakusudia kuhakikisha chanjo zinapatikana kwa kila mtu na kwa gharama nafuu.

Ghana imekuwa nchi ya kwanza duniani na barani Afrika kupokea chanjo dhidi ya virusi vya Corona chini ya programu maalum ya COVAX inayosimamiwa na Umoja wa Mataifa (UN) inakusudia kuhakikisha chanjo zinapatikana kwa kila mtu na kwa gharama nafuu.

Hatua hiyo inakuja baada ya Waghana zaidi ya 80,700 kuambukizwa ugonjwa huo na zaidi ya 580 kufariki dunia, hatimaye mwelekeo wa kuondokana na janga hilo umeanza kuonekana nchini humo. 

Shehena ya kwanza ya chanjo aina ya AstraZeneca / Oxford zilizotolewa na COVAX imewasili nchini humo jana Februari 24, 2020.

“Chanjo hizo 600,000 ni sehemu ya mpango wa awali ya kusambaza chanjo kupitia mfumo wa COVAX na zimetokana na leseni kwa taasisi ya Serum ya India na inawakilisha awamu ya kwanza ya chanjo za COVID-19 zinazoelekezwa nchi za kipato cha chini na kati,” amesema mwakilishi wa shirika la kuhudumia watoto (UNICEF) nchini Ghana, Dk Francis Kasolo baada ya shehena hiyo kuwasili. 


Zinazohusiana:


Akihojiwa na redio ya Umoja wa Mataifa, Dk Kasolo amesema kuwa njia pekee ya kuondokana na janga hili ni kuhakikisha chanjo zinapatikana kwa kila mtu popote aliko.

Kuwasili kwa shehena hiyo pia ni mwanzo wa operesheni kubwa zaidi ya kusambaza chanjo duniani ili kuokoa maisha ya watu na uchumi wa dunia.

Mfumo wa COVAX unapanga kusambaza takribani chanjo bilioni 2 za chanjo dhidi ya COVID-19 mwaka huu pekee huku malengo ni kumfikia kila mkazi wa dunia.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
26 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

Nukta TV

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

Nukta TV

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

Nukta TV