Corona: Maswali matano ya kujiuliza wakati unathibitisha habari picha yenye mshaka

March 17, 2021 6:29 am · Daniel
Share
Tweet
Copy Link
  • Maswali hayo ni pamoja na picha hiyo inahusu nini? Nani ametengeneza? Inamaanisha nini?
  • Kujibu maswali hayo kunakusaidia kukwepa mtego wa habari za uzushi kuhusu Corona. 

Dar es Salaam. Habari picha zimekuwa zikitumika kufikisha ujumbe lakini pia zinatumiwa kupotosha kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo janga la Corona. 

Licha ya kuwepo zana mbalimbali za kidijitali za uthibitishaji wa habari picha ikiwemo Google Image Reverse, TinEye, InVid na Yandex, bado ipo haya ya mtu kujiuliza maswali kadhaa kwa kila picha anayokutana nayo mtandaoni kuhusu Corona kabla ya kuisambaza.

Maswali hayo yanaweza kumsaidia kung’amua kwa urahisi habari picha inayopotosha kabla hata ya kutumia zana za kidijitali. 

Taasisi ya uthibitishaji habari ya First Draft imekuja na kanuni ambayo ipo katika mfumo wa maswali 20 ambayo unapaswa kujiuliza kabla ya kutumia au kufanya maamuzi kuhusu picha uliyoiona mtandaoni kuhusu janga la Corona.

Hata hivyo, leo tunaangazia maswali matano ya msingi:

1. Ni nini?

2. Inaonyesha nini?

3. Ni nani aliyeitengeneza?

4. Ilimaanisha nini?

5. Inamaanisha nini?


Zinazohusiana


Ukitazama swali la kwanza hadi la tatu majibu yake yanaweza kufanana kwa sababu yote haya yanajaribu kujibu ni aina gani ya picha na picha hiyo inajaribu kuonyesha nini na nani anahusika nayo. 

Ukipata majibu hayo ni rahisi kufahamu kuwa kama picha hiyo inapotosha. Mfano, umepata habari picha inayoonyesha mtu anachomwa sindano ya chanjo ya Corona, katika majibu ya maswali yako utafahamu picha inahusu chanjo ya Corona.

Lakini unatakiwa kufahamu nani kaitengeneza au kaipiga. Hapa utapata majibu kama muhusika ni chanzo cha kuaminika au la! Pia ni kweli inahusu chanjo ya Corona au ni kitu kingine. 

​Katika maswali hayo unaweza kutumia zana za kidijitali ikiwemo Google Image kupata majibu.

Swali la nne na la tano, linakupa fursa ya kukuna kichwa kubaini aliyetuma picha anamaanisha nini?, lengo lake nini? Anataka kuhabarisha au kupotosha umma?

Hapa ndipo unatakiwa kutulia na kutumia uwezo na ujuzi wako kujibu maswali hayo ili usiingie kwenye mtego wa kutumia au kusambaza uzushi kwa watu wengine na kusababisha madhara.

Ukiweza kujibu maswali hayo matano ni dhahiri utaweza kuwalinda ndugu na marafiki dhidi ya upotoshaji unaofanywa kuhusu COVID-19. 

Wakati wote ukipokea picha mtandaoni ihoji uhalali wake ili kujiweka salama wakati huu ambao duniani inapambana na janga la Corona.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV