Filamu ya ‘Binti’ yaibua vipaji vipya “bongo movie”

April 16, 2021 11:36 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni filamu ambayo imeongelea maisha ya mwanamke wa Kitanzania kwa herufi kubwa
  • Imesheheni mafunzo ya familia, mahusiano na utafutaji wa mwanamke.
  • Imetambulisha sokoni vipaji vipya katika tasnia ya uigizaji.

Dar es Salaam. Bila shaka kuna mambo mengi yanayokusubiri kufanya hasa kama ni mwanamke katika jamii ya Kiafrika. Wanawake wanaweza kulijibu na kulithibitisha jambo hilo. 

Kwa mwanamke, utalazimika kufanya mengi ikiwemo kulea familia, kufanya kazi ili kuchangia kipato cha familia, kupingana na mfumo dume ili kufikia malengo yako bila kutumia mwili wako na mengine mengi ambayo wanawake hawasimulii.

Hayo yote yamekuwa ni sehemu ya masuala yaliyoandikwa kwa herufi kubwa katika filamu ya inayoendwa kwa jina la “Binti” ambayo inaonyesha hadithi ya upambanaji wa wanawake wanne wanaolazimika kufanya mapinduzi ya maisha yao.

Filamu hiyo iliyosheheni nyota wageni katika tasnia ya filamu Tanzania wakiwemo Godliver Gordian, Helen Hartman, Jonas Mugabe na Bertha Robert imetengenezwa chini ya Seko Shamte, mwana dada ambaye ndiye mwandishi na kiongozi wa filamu hiyo.


Soma zaidi:


“Binti” imesheheni mafundisho ya unyanyapaa wa watoto wanaoishi na mahitaji maalumu, changamoto za mahusiano na mapambano ya wanamke katika kujikwamua kiuchumi.

Kwa muda, filamu hiyo imekuwa ikionyeshwa katika kumbi za kuangalizia filamu za Century Cinemax na jana ilikuwa ni tamati ya filamu hiyo katika kumbi hizo. 

Hata hivyo, filamu hiyo inaendelea kuonyeshwa katika skrini za sinema mbalimbali nchini Tanzania ikiwemo Regalz Cinemax ya Arusha.

Shamte ameiambia Nukta kuwa, mwisho wa filamu hiyo kuonyeshwa katika skrini za Century Cinemax ulikuwa ni jana (Aprili 15) lakini yeye na timu yake wanapambana kuongezewa muda ili kuwafikia watu wengi kwa sababu imeonyesha muitikio mzuri. 

Unasubiri kuitazama filamu hii ya kitanzania yenye mengi yatakayokuacha mdomo wazi. Ujachelewa changamkia fursa hiyo tazama kionjo cha filamu hiyo hapa:

                     

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
26 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

Nukta TV

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

Nukta TV

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

Nukta TV