Ripoti: Madhara ya Corona yangepungua kama tungechukua tahadhari mapema

May 13, 2021 5:36 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa (UN) ya matarajio ya ukuaji wa uchumi. 
  • Yasema wananchi na viongozi kutozingatia maelekezo ya wataalam wa afya kumezidisha athari za ugonjwa huo. 

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa (UN) imeeleza kuwa madhara ambayo dunia imeyapata hasa ya kiuchumi yaliyotokana na janga la virusi vya corona yangeweza kuzuilika iwapo Serikali za nchi zingechukua hatua za haraka mara baada ya kuripotiwa kisa cha kwanza cha Covid-19. 

Ripoti hiyo ya hali na matarajio ya uchumi duniani (WESP) iliyotolewa Mei 11 mwaka huu imesema maamuzi yasiyofaa dhidi ya Corona yamesababisha vifo vya watu 3.3 duniani na kuvuruga uchumi wa dunia.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kushindwa kwa serikali duniani kuweka mifumo thabiti na baadhi ya viongozi kupuuza kitisho cha janga la corona kulichangia kwa sehemu kubwa wananchi kutozingatia maelekezo ya wataalamu wa afya ya kujikinga na ugonjwa huo ikiwemo kuvaa barakoa. 


Soma zaidi: 


Hata hivyo, imesema kufuatia kusinyaa kwa uchumi kwa asilimia 3.6 mwaka 2020, uchumi wa dunia unatarajiwa kupanuka kwa asilimia 5.4 mwaka 2021 kutokana na hatua mbalimbali za dharura zilizochukuliwa ikiwemo utoaji wa chanjo.  

Ripoti hiyo imependekeza mfumo wa dunia wa kutoa tahadhari kufanyiwa mageuzi makubwa kwa lengo la kuepusha janga kama la Corona kutokea tena.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
13 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
13 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV