Uzushi: Siyo kweli waliopatiwa chanjo ya Corona wanafariki Uganda

June 22, 2021 10:58 am · Daniel
Share
Tweet
Copy Link
  • Kuna habari inasambaa mtandaoni ikidai waliopatiwa chanjo ya Corona wanaambukizwa kwa kasi ugonjwa huo na wanaishi kufa.
  • Wizara ya Afya Uganda yasema habari hiyo haina ukweli wowote.
  • Wananchi watakiwa kupata taarifa za chanjo ya Corona kwenye vyanzo vya uhakika.

Dar es Salaam. Kama ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii hasa WhatsApp nchini Tanzania, bila shaka umekutana na habari picha inayesema Waziri wa Afya wa Uganda ana hofu kutoka na ongezeko kubwa la wagonjwa COVID-19 nchini humo wakiwemo waliopatiwa chanjo ya corona.

Fahamu kuwa habari hiyo haina ukweli wowote na ni ya kupuuzwa kwa sababu hakuna taarifa rasmi kutoka kwa Serikali ya Uganda kuhusu ongezeko la wagonjwa na madhara ya matumizi ya chanjo ya COVID-19.

Habari hiyo imeandikwa kwa lugha ya Kiingereza inaeleza kuwa “Ministry of Health worried about the rapid infection of Covid-19 among the #Vaccinated People in Uganda whom the Ministry says are infected quickly and it’s difficult for them to get healed ending up dying.It’s time for us Trust Only God to protect us from Covid19”

Kwa tafisri isiyo ya rasmi ni kuwa habari hiyo hiyo inadai kuwa Wizara ya Afya ya Uganda inahofia maambukizi ya kasi ya COVID-19 miongoni mwa watu waliopata chanjo ya ugonjwa huo kwa sababu wanaambukizwa kwa kasi na ni vigumu kwa wao kupona na wanaishia kufariki na kuhimiza watu kumtegemea Mungu pekee.

Ukweli uko wapi?

Habari hiyo haina ukweli wowote kwa sababu Waziri wa Afya wa nchini Uganda Dk Jane Ruth Aceng Ocero hajatoa tamko kama hilo katika siku za hivi karibuni.

Vilie vile Wizara  ya Afya kupitia ukurasa wake wa Twitter imesema watu waipuze habari hiyo kwa sababu haina ukweli wowote.


Uganda alianza zoezi la kutoa chanjo dhidi ya virusi vya Corona Machi mwaka huu kwa wafanyakazi wa afya na Serikali. Uganda imepokea shehena ya dozi ya chanjo ya Corona aina ya Astra Zeneca zaidi ya 864,000.

Tangu viongozi wa dunia na wataalam waanze kutoa chanjo ya Corona, wahalifu wamejitokeza kupotosha watu kuhusu matumizi ya chanjo hiyo kwa nia ya kuzua taharuki ili kuzidisha madhara ya janga hilo kwenye jamii.

Kama ilivyo kwa Uganda, wananchi wa Tanzania wanahimizwa kupata taarifa za uhakika za chanjo ya Corona kupitia mamlaka za afya za Serikali ambazo ndiyo zimepewa mamlaka ya kuzungumzia suala hilo.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW