Faida inazopata nchi, watu wake wakipata chanjo ya Corona
- Inafungua fursa kwa watu kusafiri na kufanya biashara.
- Inapunguza vifo na kupata nguvukazi ya uzalishaji mali.
Dar es Salaam. Chanjo ya ugonjwa wa Corona ni kati ya njia zilizoonekana kuchukua nafasi kubwa katika kupambana na ugonjwa huo kwa sasa duniani.
Kwa sasa chanjo sita ikiwemo Moderna zimeidhinishwa na zinatolewa kwa nchi mbalimbali ili kukabiliana na virusi hivyo ambavyo vimeathiri maisha na uchumia wa dunia.
Kutolewa kwa chanjo ya Corona kumesaidia kulegezwa kwa masharti yaliyowekwa awali kukabiliana na ugonjwa huo ikiwemo kuzuiliwa kwa safari za kimataifa na watu kutoruhusiwa kutoka katika nyumba zao (lockdown).
Ni faida gani nyingine ambazo nchi inaweza kupata endapo watu wake watapatiwa chanjo dhidi ya Corona.
Katika video hii, Nukta Fakti inakuletea faida ambazo zinaambatana na nchi kukubali kupokea chanjo dhidi ya Corona:
        Â
Latest