Kwa nini ubadilishe mswaki baada ya kupona Corona?

July 28, 2021 10:35 am · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Virusi vinaweza kubaki kwenye mswaki wa zamani na kuibua maambukizi mapya.
  • Endapo mtu hana uwezo wa kupata mswaki mpya anashauriwa kusafisha kwa maji ya moto.

Dar es Salaam. Kama ulishapata maambukizi ya virusi vya Corona (Uviko-19) na kupona unahitaji ufafanuzi juu ya dhana ya kuachana na mswaki uliokuwa ukiutumia wakati unaumwa ili kuepuka maambukizi mapya ya ugonjwa huo.

Hilo linatokana na kuwepo kwa mjadala kwenye mitandao ya kijamii ambao baadhi ya watu wanasema ni sahihi na wengine wakisema siyo sahihi kuacha kutumia mswaki ambao ulikuwa ukitumia wakati umepata Uviko-19.

Moja ya taarifa hizo zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii hasa Whatsapp imebeba kichwa cha habari “COVID RECOVERED SHOULD CHANGE TOOTHBRUSH” ikimaanisha kuwa “waliopona COVID-19 wabadilishe miswaki”

Moja ya ujumbe unaowataka watu kubadilisha miswaki mara baada ya kupona Uviko-19, njia mbayo imependekezwa na baadhi ya wataalam wa afya. Picha| Matandao.

Ni sahihi kutumia mswaki mpya baada ya kupona?

Kwa mujibu wa Dr Pravesh Mehra kutoka India anasema uwezekano wa mtu kupata maambukizi kwa mara nyingine endapo atatumia mswaki aliokua akitumia akiwa na maambukizi ni mkubwa kwa sababu vijidudu vinakua vimebaki kwenye kifaa hicho cha kusafishia meno.

Hivyo inashauriwa mtu kubadili mswaki mara baada ya kupona Corona.

“Kama wewe au yeyote kwenye familia yako amepata Corona, akipona hakikisha anabadilisha mswaki au vitakasa mdomo.  Miswaki inaweza kubakisha virusi na njia sahihi ya kuwaondoa ni kwa kubadili mswaki,” anasema Dr Mehra.

Sababu kuu ya kutumia mswaki ni kuepuka virusi ambavyo zinaweza kuwa vimebaki kwenye mswaki, jambo linaloweza kumuweka mtu aliyepona katika hatari ya kupata tena maambukizi.

Daktari wa kinywa na meno kutoka hospitali ya Meno Yangu ya jijini Dar es Salaam, Dk Esther Emmanuel amesema hana uhakika na dhana hiyo ila anafikiri hiyo ni njia sahihi ya kukabiliana na maambukizi mapya ya Uviko-19 kwa mtu aliyepona. 

“Tunashauri mgonjwa wa Corona atumie mswaki mpya pale anapoweza. Kama hatakua na uwezo huo ni vyema kusafisha mswaki wa awali kwa maji ya moto ili kuuwa virusi vinavyobaki kwenye mswaki wa zamani,” anasema Dk Esther.

Daktari huyo amesema ushauri huo hutolewa hata kwa watu waliopona magonjwa mengine ikiwemo ya kinywa ili kuwaweka salama zaidi.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
23 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
24 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
24 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Baba Levo: Wazo la kuongeza tozo kwenye bodaboda litolewe, tuleteeni watu wa tungi

Baba Levo: Wazo la kuongeza tozo kwenye bodaboda litolewe, tuleteeni watu wa tungi

Nukta TV

Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Nukta TV

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Nukta TV