WHO yazindua mkakati mpya usambazaji chanjo ya Uviko-19 duniani

October 8, 2021 8:59 am · Herimina
Share
Tweet
Copy Link
  • Yaweka mpango wa utoaji chanjo kwa asilimia 70 ya wakazi duniani.
  • Nchi zinazotengeneza chanjo kuruhusu usafirishaji wa chanjo kwenda nchi nyingine.
  • Elimu na hamasa kutolewa zaidi kufikia lengo hilo.

Dar es Salaam. Wakati juhudi za utoaji chanjo zikiendelea duniani, Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) limezindua mkakati wa kufikisha chanjo ya Uviko-19 kwa asilimia 70 ya wakazi wa dunia ifikapo katikati ya mwaka 2022.

Mkakati huo uliozinduliwa Oktoba 7 mwaka huu, una lengo la kumaliza mwenendo hafifu wa utoaji chanjo hizo duniani.

Lengo la awali la Shirika hilo, lilikuwa ni kuona asilimia 10 ya wakazi wa kila nchi wawe wamechanjwa chanjo ya Uviko-19 katikati ya mwezi wa Septemba mwaka huu, lakini nchi 56 hazijafikia lengo hilo, huku nyingi zikiwemo barani Afrika na Mashariki ya mbali.

Mkakati huo mpya unaweka mipango ya WHO kuchanja asilimia 40 ya wakazi wa kila nchi ifikapo mwisho wa mwaka huu wa 2021 na asilimia 70 katikati ya mwaka ujao wa 2022.

WHO yaweka mpango wa kuchanja asilimia 40 ya wakazi wa kila nchi ifikapo mwisho wa mwaka 2021. Picha|  istockphoto.com.

Akizungumza katika uzinduzi wa mkakati huo, Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dk Tedros Ghebreyesus amesema kuwa  dunia inaweza kufikia lengo hilo lakini kinachotakiwa ni utashi na uongozi wa kisiasa, na kuongezwa kwa hatua na ushirikiano zaidi ya kile kilichoshuhudia hivi sasa.

Ili kufanikisha utoaji chanjo kwa kiwango pendekezwa, mkakati unaweka hatua tatu za utoaji chanjo kwa kila nchi, ikiwemo chanjo kwa wazee, wahudumu wa afya na  makundi yaliyo hatarini zaidi, vilevile chanjo kwa kundi la watu wazima na vijana. 

Mkakati umeelekeza nchi zinazotengeneza chanjo kuruhusu usafirishaji wa chanjo hizo kwenda nchi nyingine, huku kampuni zinazotengeneza chanjo hizo zikitakiwa kupatia kipaumbele upelekekaji wa chanjo hizo kupitia majukwaa ya kusaka na kusambaza chanjo likiwemo la  COVAX la Umoja wa Mataifa na AVAT la Muungano wa Afrika. 

Vilevile, asasi za kiraia na kijamii zimetakiwa kutumia uwezo wao kupigia chepuo upatikanaji sawa wa chanjo na kuelimisha umma juu ya umuhimu wa chanjo hasa kuondokana na fikra potofu kuhusu chanjo ya Corona.

Hadi Oktoba 6, ni dozi bilioni 6.3 zimeshatolewa duniani kote, huku dozi bilioni 11 zikihitajika ili kufikia mkakati wa chanjo kwa asilimia 70 ya wakazi wa dunia ifikapo katikati ya mwaka 2022.  

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV