Corona: Katavi yapata Sh2.33 bilioni miradi ya maji

November 23, 2021 3:55 am · Herimina
Share
Tweet
Copy Link

Dar es Salaam. Shirika la Fedha Duniani (IMF) liliipatia Tanzania mkopo wa dharura wa Dola za Marekani milioni 567.25 (Sh1.3 trilioni) kwa ajili ya kukabiliana na athari za ugonjwa wa Corona (Uviko-19).

Taarifa ya IMF iliyotolewa Septemba 7 mwaka huu ilisema bodi ya shirika hilo imeidhinisha kutolewa kwa kiasi hicho cha fedha ambapo kitaisaidia Tanzania katika kuhimili mahitaji yatokanayo na janga la Uviko-19.

IMF ilieleza kuwa uchumi wa Tanzania ulitikisika  kutokana na athari za Uviko-19, hivyo msaada wa kifedha ni muhimu kuurejesha katika hali ya kawaida.

Kati ya fedha hizo, Wizara ya Maji alipewa Sh139.4 bilioni ili kutekeleza miradi 218 katika Halmashauri mbalimbali ili kuboresha miundombinu ya maji ili kuwapunguzia wananchi makali ya Uviko-19 katika sekta ya maji.

Kati ya fedha hizo Mkoa wa Katavi umepata Sh2.33 bilioni kutekeleza miradi mitatu kama inavyoonekana katika infografia hii.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV

Sakata bei ya mafuta kupanda latua BoT, Naibu Gavana atoa ufafanuzi

Sakata bei ya mafuta kupanda latua BoT, Naibu Gavana atoa ufafanuzi

Nukta TV

BoT yabakiza Riba ya Benki Kuu 5.75% kudhibiti mfumuko wa bei

BoT yabakiza Riba ya Benki Kuu 5.75% kudhibiti mfumuko wa bei

Nukta TV