Infografiki: Namna fedha za IMF zilivyogawanywa miradi ya maji Kigoma

November 23, 2021 7:33 am · Herimina
Share
Tweet
Copy Link
  • Mkoa wa Kigoma ni moja ya mikoa iliyobahatika kupata fedha kugharamia miradi ya maji ili kukabiliana na Uviko-19
  • Sehemu kubwa ya thamani ya miradi hiyo ya maji inafanana huku wilaya ya Kakonko ikiwa na kiwango kikubwa kidogo

Dar es Salaam. Shirika la Fedha Duniani (IMF) liliipatia Tanzania mkopo wa dharura wa Dola za Marekani milioni 567.25 (Sh1.3 trilioni) kwa ajili ya kukabiliana na athari za ugonjwa wa Corona (Uviko-19) ikiwemo kutatua huduma za kijamii ambazo ni muhimu kukabiliana na janga hilo lililogharimu maisha ya watu zaidi ya milioni tano ulimwenguni.  

Taarifa ya IMF iliyotolewa Septemba 7 mwaka huu ilisema bodi ya shirika hilo imeidhinisha kutolewa kwa kiasi hicho cha fedha kitachoisaidia Tanzania katika kuhimili mahitaji yatokanayo na Uviko-19 ikiwemo kuuimarisha uchumi uliokuwa umeathirika na janga hilo kuanzia Machi, 2020. 

Katika matumizi ya fedha hizo za IMF, Tanzania ilizigawanya katika sekta mbalimbali zikiwemo za afya, elimu na maji. 

Kati ya fedha hizo, Wizara ya Maji ilipewa Sh139.4 bilioni ili kutekeleza miradi 218 katika halmashauri mbalimbali ili kuboresha miundombinu ya maji  kwa kuwapunguzia wananchi makali ya Uviko-19 kutokana na uhaba wa huduma hiyo. 

Mkoa wa Kigoma umepata Sh3.48 bilioni kutekeleza miradi saba ya maji itakayowafanya wakazi wa eneo hilo la magharibi mwa Tanzania kuwa na uhakika wa kunawa kwa sabuni na maji tiririka ambayo ni moja ya afua muhimu za kukabiliana na Uviko-19. 

Je, ni miradi ipi hiyo inayotekelezwa na fedha za IMF mkoani Kigoma? 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
14 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
14 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV