Tanzania yapokea dozi 115,200 za chanjo ya Janssen

December 3, 2021 2:26 pm · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link

Dar es Salaam. Tanzania imepokea shehena ya chanjo ya aina ya Janssen dozi 115,200 kutoka Serikali ya Ubeligiji kupitia mpango wa COVAX Facility itakayosaidia kuimarisha mapambano ya Uviko-19 nchini.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Dorothy Gwajima amesema kuwa Serikali itaendelea kutoa chanjo dhidi ya Uviko-19 katika vituo mbalimbali vya afya ili kuwakinga wananchi.

Dozi hizo zimepokolewa katika uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam kutoka kwa Balozi wa Ubeligiji nchini Tanzania, Peter Van Acker.

Kwa mujibu wa Dk Gwajima, awamu ya kwanza Serikali ilipokea dozi milioni 1.05, awamu ya pili dozi 169,000 na leo Desemba 3, 2021 imepokea 115,200 hivyo kufanya jumla ya Chanjo aina ya Janssen zilizopokelewa hapa nchini kufikia dozi milioni 1.34.

Hiyo inafanya jumla ya chanjo zote zilizopokelewa nchini mpaka sasa kufikia dozi milioni 4.42 zikiwemo chanjo ya Sinopharm na Pfizer ambazo zitachanja watu milioni 2.88. 

Aidha, Dk Gwajima amewaagiza viongozi na watendaji wa ngazi zote kutoa ushirikiano wa hali ya juu na kuhamasisha jamii kujitokeza kupata chanjo na  kisha kujikinga kwa kuchukua tahadhari dhidi ya Uviko 19. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
24 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
24 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Baba Levo: Wazo la kuongeza tozo kwenye bodaboda litolewe, tuleteeni watu wa tungi

Baba Levo: Wazo la kuongeza tozo kwenye bodaboda litolewe, tuleteeni watu wa tungi

Nukta TV

Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Nukta TV

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Nukta TV