Mwelekeo wa Serikali ya Rais Samia mwaka 2022

January 1, 2022 7:40 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni kukabiliana na changamoto za wananchi.
  • Kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja.
  • Kuendeleza mapambano dhidi ya janga la Uviko-19.

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameanika mipango ya Serikali yake kuelekea mwaka 2022 ambayo imejikita katika kuimarisha ustawi wa Watanzania kiafya na kiuchumi.

Rais Samia amesema hayo wakati akihutubia Watanzania kwa njia ya televisheni leo Desemba 31, 2022.

Amesema 2022 ni mwaka wa kukabiliana na changamoto zinazopunguza uwezo wa wananchi katika kukabiliana na maisha ya kila siku ili kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na wa Taifa kwa ujumla.

Amesema dunia inakabiliwa na ugonjwa wa Corona (Uviko-19) na itaendeleza mapambano ya ugonjwa huku akiwataka wananchi kuchukua tahadhari kwa sababu wimbi la nne la ugonjwa huo na kirusi cha Omicron tayari kimeshaingia Tanzania.

“Nitumie fursa hii kuwahimiza wananchi kupata chanjo dhidi ya Uviko 19, natambua kuwa chanjo haizuii mtu kupata maambukizi ila inapunguza makali ya ugonjwa huu. Hivyo niwakumbushe wananchi kwenda, chanjo zipo na zinapatikana bila malipo,” amesema Rais.


Soma zaidi:


Eneo lingine litakalopewa kipaumbele na Serikali ya Tanzania ni kuhakikisha zoezi la Sensa ya Watu na Makazi linafanikiwa kwa kuhakikisha watu wote wanahesabiwa ili kupata takwimu zitakazosaidia kufanya maamuzi sahihi ya maendeleo.

Amesema sensa itasaidia upatikanaji wa takwimu zitakazosaidia serikali kupanga kwa usahihi mipango ya maendeleo.

“Ni vyema tukauanza mwaka mpya2022 na lengo la kuongeza ufanisi katika uzalishaji na ubora katika kutoa huduma,” amesema Rais Samia akiwasihi wafanyakazi wa sekta ya umma na binafsi.


Wito kwa wazazi

Amewataka wazazi kutokubweteka na msimu wa sikukuu na sherehe zake na badala yake kuwaandaa watoto wao kukabiliana na changamoto za masomo katika mwaka u ujao ili waweze kunufaika na elimu inayotolewa.

Amewataka wanaosafiri msimu huu wa mwisho wa mwaka kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali na kuokoa nguvukazi ya Taifa inayotegemewa katika uzalishaji.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW