Mussa Zungu achaguliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la Tanzania

February 11, 2022 1:18 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Amepigiwa kura za ndiyo 296
  • Alikuwa mgombea pekee katika nafsi hiyo.
  • Anachukua nafasi Dk Tulia Ackson aliyechaguliwa kuwa Spika.

Dar es Salaam. Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu amechaguliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la Tanzania baada ya Wabunge kumpigia kura za ndiyo 296 Kati ya 301.

Zungu aliyepitishwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea nafasi ya hiyo anaichukua nafasi ya Dk Tulia Ackson ambaye alichaguliwa kuwa Spika wa Bunge.

Dk Tulia ameziba nafasi iliyoachwa wazi na Job Ndugai aliyejiuzulu Januari 6 mwaka huu baada ya kuwepo shinikizo kubwa kutoka kwa watu mbalimbali la kumtaka kujiuzulu kutokana na kauli yake iliyokosoa uamuzi wa Serikali kukopa zaidi mikopo kugharamia miradi ya maendeleo.

Zungu amekuwa Mwenyekiti wa Bunge tangu Bunge la 10 akimsaidia aliyekuwa Spika wa wakati huo Anne Makinda na ameendelea na nafasi hiyo hadi alipochaguliwa kuwa Naibu Spika.

Kwa nyakati tofauti wakati akiongoza vikao vya Bunge amekuwa akionekana kukimudu kiti hasa pale panapokuwa na mivutano ya wabunge kuhusu hoja mbalimbali. 

Zungu ameahidi kushirikiana na wabunge wote katika kuleta mstakabari mzuri kwa Taifa. Picha| Mtandao.

Akizungumza baada ya kuchaguliwa, Zungu amewashukuru Wabunge kwa kumwamini na kumchagua katika nafsi hiyo na ameahidi kutimiza majukumu yake kwa mujibu wa sheria ikiwemo kuisimamia Serikali ili kuwaletea wananchi maendeleo.

Baada ya kiapo, Zungu ameahidi kushirikiana na wabunge na kufanya kazi nao ili kuleta mstakabadhi wa kujenga taifa la Tanzania.

“Siasa zikitoka kwenye uchaguzi zinarudi bungeni na bungeni ni kushirikiana na miradi ya serikali kuhakikisha pesa zilizotoa serikali zinasimamiwa vizuri kwenye halmashauri zetu,” amesema Zungu.

Katika taarifa iliyotolewa Februari 10, 2022 na Idara ya Habari ya Bunge ambayo ilisainiwa na na Katibu wa Bunge, Nenelwa Mwihambi, ilionyesha hakuna chama kingine cha siasa chenye uwakilishi bungeni ambacho kilipeleka jina la mgombea na hivyo kumfanya Zungu kuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo. 

Kanuni za Bunge zinataka Naibu Spika atokane na mbunge aliyeko bungeni ambapo Bunge la 12. Vyama ambavyo vina wabunge katika Bunge hilo ni CCM, Chadema, CUF na ACT Wazalendo.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV