Snapchat kuwapa shavu tena watumiaji wake

February 16, 2022 7:14 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Itanza kuwalipa watu wenye wenye maudhui yanayoangaliwa na watu wengi.
  • Malipo hayo yatatokana na matangazo kwenye maudhui ya watu.
  • Ni njia rahisi kwa vijana kujipatia pesa.

Dar es Salaam. Huenda tatizo la ajira likapungua kadri siku zinavyoendelea kwani mitandao ya kijamii inafugulia fursa watumiaji wake kupata fedha kwa njia ya mtandao.

Kutoka Facebook, Instagram, Twitter, TikTok na sasa Snapchat ni mwendo wa watengeneza maudhui kupiga pesa mtandaoni. Inawezekanaje ukapata pesa kwa kuchapisha maudhui mtandaoni?

Snapchat, mtandao wa kijamii wa kupakia picha na video hivi karibuni umetangaza kuweka matangazo kwenye picha na video za watengeneza maudhui na kugawana nao fedha inayopatikana.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la The Verge, ili mtu anufaike na malipo hayo, Snapchat itazingatia mwenendo wa mtu kupakia maudhui pamoja na watu wanavyochangamana na maudhui au mambo anayoweka katika mtandao huo.

Siyo kwa wote

Ili kufikiwa na huduma hiyo, Snapchat imesema vipo vigezo vya kuzingatiwa. Kigezo cha kwanza ni kuwa, mtu anatakiwa kuwa mashughuli kwenye mtandao huo na mwenye wafuasi wengi.

Hiyo ni imani ya kuwa, endapo Snapchat itaweka matangazo kwenye stori za mtu, ni lazima tangazo litawafikie watu wengi zaidi.

Hatua hiyo imefikiwa na mtandao huo baada ya watu kupunguza muda wao kwenye programu tumishi (app) hiyo.


Soma zaidi


Mkurugenzi Mtendaji wa Snapchat, Evan Spiegel amesema hivi karibuni, watu wamepunguza muda wao kwenye App ya Snapchat na badala yake wanatazama maudhui katika mtandao wa TikTok.

Snapchat haijaanza leo kutoa ofa kama hizo. Imeanza tangu mwaka 2020 ambapo ilitangaza kuanza kulipa watengeneza maudhui mtandaoni.

“Kwa mwaka 2021, Snapchat imelipa zaidi ya Sh578 bilioni kwa watoa maudhui,” imesomeka habari ya The Verge.

/
No matches found for this filter
31 May, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
31 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
31 May, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

Nukta TV

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

Nukta TV

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

Nukta TV