Rasmi: Apple kuisambaratisha iTunes

June 5, 2019 7:09 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link

Apple inamaliza minong’ono iliyokuwepo juu ya mpango wa kampuni hiyo kubwa duniani kuivunja huduma hiyo hasa baada ya kuwepo ushindani mkali katika tasnia hiyo. Picha|Mtandao.


  • Kwa sasa iTunes itagawanywa katika programu tumishi (Apps) tatu za video, muziki na muziki wa mtandaoni.  
  • Apple inahamia kuelekea kuwa mtoa huduma wa burudani mbalimbali, badala ya kuwa mtoa huduma wa vifaa vya kielektroniki pekee.
  • Nafasi ya iTune itachukuliwa na programu nyingine ya  MacOS Catalina.

Watumiaji huduma za iTunes kupata muziki, sasa wajiandae kuanza kutumia huduma tofauti na waliozoea baada ya iTunes kuvunjwa na kihitimisha safari ya miaka 18 ya kuwepo sokoni na kuwatoa wengi katika ulimwengu wa muziki.

Kampuni ya Apple ya Marekani inayotengeneza simu za Iphone imetangaza kuivunja programu yake tumishi ya iTunes iliyokuwa inatumika kama soko la muziki la mtandaoni katika mkutano uliofanyika California, Marekani hivi karibuni. 

Nafasi ya programu hiyo itachukuliwa na programu nyingine ya  MacOS Catalina ambayo Apple imeitambulisha tayari ambapo kwa sasa iTunes itagawanywa katika programu tumishi (Apps) tatu za video, muziki na muziki wa mtandaoni.  

Ina maana watumiaji wanaweza kutarajia programu mpya ya muziki ili kutoa kile ambacho iTunes hufanya sasa, lakini kwa interface (muonekano) bora.


Soma zaidi: 


Kwa kutenganisha huduma zake, Apple inahamia kuelekea kuwa mtoa huduma wa burudani mbalimbali, badala ya kuwa mtoa huduma wa vifaa vya kielektroniki pekee.

Taarifa hiyo ya Apple inamaliza minong’ono iliyokuwepo juu ya mpango wa kampuni hiyo kubwa duniani kuivunja huduma hiyo hasa baada ya kuwepo ushindani mkali katika tasnia hiyo.

Ujio wa huduma za muziki mtandaoni kama Tidal na Spotify ulishusha pia umaarufu wa huduma za iTunes na huenda mpango mpya wa Apple ukaisaidia kuongeza mapato katika nyanja hizo na kuimarisha ushindani.

Enable Notifications OK No thanks