Fedha za Uviko-19 zilivyochangia kupanda kwa bajeti ya 2021-22

February 19, 2022 6:43 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni Sh1.3 trilioni zilizotolewa na IMF kupambana na Uviko-19.
  • Bajeti hiyo Kuu ya Serikali imepanda hadi Sh37.9 trilioni.

Dar es Salaam. Bajeti Kuu ya Serikali ya Tanzania kwa mwaka 2021/22 imeongezeka kwa Sh1.3 trilioni hadi kufikia Sh37.9 trilioni wakati ikiwa imebaki miezi michache utekelezaji wake kufika kikomo. 

Awali bajeti hiyo iliyopitishwa na Bunge Juni mwaka 2021 ilikuwa Sh36.6 trilioni na ukomo wake wa utekelezaji utakuwa Juni mwaka huu. 

Kuongezeka kwa bajeti hiyo kumetokana na Serikali kupata mkopo usio na riba kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) wenye thamani ya Sh1.3  trilioni ambao unatumika kwa miezi tisa. 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Yusuf Masauni amesema kuwa fedha hizo hazikuwa sehemu ya bajeti iliyoidhinishwa na Bunge mwaka 2021/22.

Serikali inawajibika chini ya kifungu cha 43 cha Sheria ya Bajeti, sura 439 na Ibara ya 137 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwasilisha bungeni mapendekezo ya kuomba ridhaa ya Bunge kutumia fedha za mkopo huo.

Fedha hizo zilizotolewa na IMF zilikuwa mahususi kuwapunguzia Watanzania maumivu ya athari za janga la Uviko-19 katika sekta mbalimbali na kuchochea shughuli za kiuchumi na kijamii zilioathirika na ugonjwa huo kwa upande wa Tanzania Bara na Visiwani.

‘Kati ya kiasi hicho, Sh1.07 trilioni ni kwa ajili ya Tanzania Bara, sawa na dola za Marekani milioni 467.3 na Sh231 bilioni, sawa na dola za Marekani milioni 100 kwa ajili ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,’ amesema  Masauni.


Zinazohusiana: 


Masauni amesema kuwa mchakato wa kupata mkopo huo ulihusisha sekta mbalimbali ambapo baadhi ya sekta hazikukidhi kujumuishwa kwenye mgao wa fedha hizo kwa mujibu wa vigezo na masharti ya IMF. 

Sekta zilizokidhi vigezo hivyo ni afya, elimu, utalii, maji, biashara ndogo ndogo kupitia makundi maalum ya vijana, wanawake na wenye ulemavu na kaya maskini kupitia mfuko wa hifadhi ya jamii (TASAF).

Matumizi ya fedha hizo yamegawanywa kulingana na vipaumbele ilivyojiwekea Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/22 ambapo sekta ya afya ilipata Sh466.9 bilioni na sekta ya elimu Sh368.9 bilioni.

Sekta ya maji ilipata Sh139.4 bilioni, sekta ya utalii (Sh90.2 bilioni) na TASAF Sh5.5 bilioni.

Almewahakikishia Wabunge kuwa fedha hizo zitatumika na kusimamiwa kikamilifu na Serikali na kumtaka Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) kufuatilia matumizi ya fedha hizo ili kuzuia ubadhilifu wakati wa utekelezaji wa miradi iliyoanishwa kutekelezwa kwa kutumia fedha hizo.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
25 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
25 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

Nukta TV

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

Nukta TV

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

Nukta TV