Congo DRC, Burundi zaungana na Tanzania ujenzi reli ya kisasa

April 30, 2022 7:29 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Zajadiliana kuchukua mkopo wa Sh2.1 trilioni kujenga reli hiyo.
  • Inajengwa kutoka Dar es Salaam- Mwanza-Kigoma hadi nchi jirani.
  • Itaongeza ufanisi wa biashara na ajira kwa wananchi.

Dar es Salaam. Wakati ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza ukiendelea, nchi za Tanzania, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (Congo DRC) ziko kwenye majadiliano kuhakikisha reli hiyo inafika nchi za maziwa makuu ili kuongeza kasi ya biashara na maendeleo ya wananchi wa nchi hizo.

Nchi za Tanzania, Burundi na Congo DRC zimewasilisha maombi ya kupatiwa mkopo wenye masharti nafuu kwenye Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Uvinza-Msongati- Gitega, yenye urefu wa kilomita 939, uliokisiwa kugharimu Dola za Marekani milioni 900 (Sh2.1 trilioni).

Majadiliano ya awali kati ya benki hiyo na mawaziri wa fedha wa nchi hizo tatu, Dk Mwigulu Nchemba wa Tanzania, Nicolas Kazadi wa DRC na Dk Domitien Ndihokubwayo wa Burundi, yamefanyika kando ya Mikutano ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) inayoendelea nchini Marekani.

Dk Nchemba akizungumza baada ya majadiliano hayo amesema kuwa reli hiyo ni muhimu kwa ustawi na maendeleo ya kiuchumi ya nchi zote tatu kwa sababu itakapokamilika itarahisha usafirishaji wa mizigo, abiria na kukuza biashara na maendeleo ya viwanda ya nchi hizo.

Kwa mujibu wa Nchemba,  mradi huo ni mkubwa ndiyo maana nchi hizo zimekubaliana kutafuta mikopo nafuu kutoka vyanzo mbalimbali na pia kwa kutumia fedha zitakazotengwa kwenye bajeti zao za ndani ili mradi huo uanze kujengwa.

Januari 2022, Serikali ya Tanzania na Burundi zilitia saini za makubaliano ya awali ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa reli ya Kisasa (SGR) kutoka Uvinza  (Tanzania) hadi Gitega, Burundi yenye urefu wa kilomita 282.


Soma zaidi:


Mkurugenzi Mtendaji wa AfDB Kanda ya Afrika Mashariki, Nnenna Nwabufo, amesema kuwa benki yake inatambua umuhimu wa mradi huo kiuchumi, kisiasa na kijamii na kwamba utasaidia pia kuziunganisha nchi nyingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki na ni muhimu kwa ajili ya utengamano wa nchi hizo.

Ameahidi kuwa benki yake itashiriki kikamilifu kuhakikisha kuwa mradi huo unajengwa kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizo pamoja na maendeleo ya kiuchumi ya nchi zinazoshiriki katika kujenga mradi huo muhimu.

Ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza na kisha Kigoma itakayounganisha nchi za maziwa makuu ikiwemo Burundi, Congo DRC na Rwanda utasaidia kuongeza ufanisi katika sekta ya usafirishaji hususani sekta ya reli ambapo itabeba mzigo wa mpaka tani 10,000 kwa mkupuo sawa na uwezo wa maroli 500 ya mizigo na kuokoa muda wa usafirishaji abiria na mizigo.

Pia itachangia katika ongezeko la ajira kwa wazawa katika sekta na fani mbalimbali na uboreshaji wa huduma za kijamii ikihusisha ujenzi wa shule, vituo vya afya na ujenzi wa barabara katika maeneo yanayopitiwa na mradi huo.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV