Tanzania ilivyojipanga kudhibiti wimbi la tano la Uviko-19

June 3, 2022 5:53 am · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Unalenga kuchanja watu 59,000 kwa siku.
  • Watanzania wahimizwa kuendelea kuchukua tahadhari kwani korona ipo.

Dar es Salaam. Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema Serikali na wadau wa maendeleo wataongeza kasi ya utoaji chanjo ili kukabiliana na tishio la wimbi la tano la ugonjwa wa Corona (Uviko-19).

Utoaji wa chanjo ya Uviko-19 utaenda sambamba na kampeni mpya yenye lengo la kuongeza kasi ya kuhamasisha jamii kupata chanjo pamoja na kufuatilia wale ambao hawakukamilisha chanjo yenye dozi mbili.

Waziri Ummy amesema kuwa kutokana na mataifa jirani ya Kenya na Afrika Kusini kuripoti ongezeko la wagonjwa wa Uviko-19, wizara yake na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) wanaongeza jitihada katika afua za kukabiliana na ugonjwa huo.

“Ugonjwa wa Uviko-19 bado upo na kwa sababu ipo hatari au tupo katika tishio la kupata wimbi la tano la mlipuko wa Uviko-19 ndiyo maana pia leo tunazindua mpango huu wa Global Vax ili kuwatayarisha Watanzania kuweza kupambana na wimbi linalokuja la Uviko-19,” amesema Ummy jana Juni 2, 2022 wakati wa uzinduzi wa  mkakati huo unaofahamika kama Global Vax.

Kasi ya kuchanja kuongezeka 

“Ninapenda kuwakumbusha kwamba ili tufikie kinga jamii (herd immunity), hapa nchini tumejiwekea malengo ya kutoa chanjo ya Uviko-19 kwa walengwa milioni 21.5 ifikapo Desemba, 2022.  Idadi hii ni sawa na asilimia 70 ya wananchi wenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea,” amesema Ummy. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
16 Aug, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
16 Aug, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
16 Aug, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia: AFCON ni fursa, wawekezaji karibuni kuwekeza

Rais Samia: AFCON ni fursa, wawekezaji karibuni kuwekeza

Nukta TV

Utani wa Rais Samia, matokeo kati ya Simba na Yanga

Utani wa Rais Samia, matokeo kati ya Simba na Yanga

Nukta TV

Rais Samia awataka wananchi wa Kizimkazi kutunza miundombinu ya maji

Rais Samia awataka wananchi wa Kizimkazi kutunza miundombinu ya maji

Nukta TV