Uviko-19 unasababisha matatizo ya neva?

September 26, 2022 12:08 pm · Davis Matambo
Share
Tweet
Copy Link
  • Baadhi ya watafiti wamesema mtu anaweza kupata magonjwa hayo.  
  • Hata hivyo, athari hizo ni za muda mrefu.               

Dar es Salaam. Huenda watu waliowahi kuugua ugonjwa wa Uviko-19 wakapata athari za kiafya za muda mrefu ikiwemo kiharusi, utafiti mpya umeeleza. 

Tafiti nyingi zilizofanywa baada ya mlipuko wa Uviko-19 zimejikita kwa wagonjwa waliolazwa hospitalini, au walioruhusiwa kwa ndani ya kipindi cha miezi sita na kushindwa kuangazia madhara ya muda mrefu ya ugonjwa huo. 

Utafiti mpya kutoka Shule ya Tiba ya Chuo Kikuu cha Washington cha Marekani uliotolewa Septemba 22 mwaka huu uliotazama matatizo ya kiafya kutokana na Uviko-19 umetoa uchunguzi wa kina zaidi hadi sasa kuhusu matatizo ya muda mrefu ya neva yanayohusiana na Uviko-19 kwa waathirika tofauti na wasiowahi kuwa na maambukizi.

Tafiti hiyo imefuatilia zaidi ya wagonjwa 150,000 wa Uviko-19 kwa miezi 12 na kugundua maambukizo yalisababisha ongezeko la asilimia 42 la hatari ya matatizo ya muda mrefu ya neva kwa wagonjwa.

Ongezeko la hatari la mfululizo wa matukio katika mfumo wa neva unajumuisha kiharusi cha kwa asilimia 50, matatizo ya utambuzi na kumbukumbu (asilimia 77), matatizo kipandauso na kifafa (asilimia 80) na shida ya macho kwa asilimia 30.

Matatizo ya afya ya akili, matatizo ya misuli, pingili za mgongo, gegedu na viungo, matatizo ya hisia, matatizo ya upumuaji na udhaifu unaoweza kusababisha kupooza kwa viungo na kuvimba katika ubongo, ambako mara nyingi hutokana na maambukizi ya virusi.

“Utafiti wetu hutoa tathmini ya kina ya matokeo ya muda mrefu ya neva ya Uviko-19…Utafiti wa zamani umechunguza seti nyembamba ya matokeo ya neva, haswa kwa wagonjwa waliolazwa hospitalini.” ameeleza Ziyad Al-Aly Mtaalamu wa magonjwa katika Chuo Kikuu cha Washington.


Soma zaidi:


Watafiti wa utafiti huo wanaeleza kuwa baadhi ya hatari za hali maalum za neva ni kubwa zaidi kwa vijana. 

“Hatari ya matatizo ya kumbukumbu na utambuzi, hisia na matatizo ya uvimbe kwenye ubongo ni makubwa kwa vijana,” Al-Aly amesema.

Kutokana na utafiti huu na hali ya kuenea kwa janga hili ulimwenguni kote ni dhahiri ongezeko jipya la wagonjwa wa Uviko-19 kunaweza kuongeza idadi ya watu wanaokumbwa na hatari ya magonjwa ya neva.

“Kwa kuzingatia kiwango kikubwa cha janga hili, na ingawa idadi kamili iliyoripotiwa katika kazi hii ni ndogo, hizi zinaweza kutafsiri kuwa idadi kubwa ya watu walioathiriwa ulimwenguni kote na hii itachangia kuongezeka kwa mzigo wa magonjwa ya neva.” watafiti waliripoti katika utafiti huo.

Kulingana na watafiti hata kupunguza idadi ya waathirika wanaokabiliwa na changamoto za ubongo kufikia nusu kutoka milioni 6 walioambukizwa Marekani pekee bado kunaacha mamilioni ya watu wakikabiliwa na changamoto hii baada ya Uviko-19.

Kwa mujibu wa Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC), Chanjo ya Uviko-19 husaidia kukulinda kwa kuongeza uwezo wa kingamwili bila wewe kukabiliwa na ugonjwa hatari au hali mbaya za baada ya uVIKO-19.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW