Usidanganywe: ‘Hydroxychloroquine’ haitibu Corona

November 22, 2022 10:46 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • WHO yasema matumizi ya dawa hiyo kutibu Corona yanaweza kusababisha magonjwa ya moyo, figo na ini.
  • Dawa hiyo ni tiba sahihi kwa ugonjwa wa malaria na aina ya kwanza ya kisukari.

Dar es Salaam. Kwa kipindi kirefu tangu kuzuka kwa ugonjwa wa Corona watu wamekuwa wakihusisha dawa ya ‘hydroxychloroquine’ na tiba ya ugonjwa huo, jambo ambalo wataalam wa afya wanasema si kweli.

Licha ya uwepo wa chanjo ya ugonjwa huo bado baadhi ya watu wanasambaza taarifa za uzushi kwamba ‘hydroxychloroquine ni tiba kamili ya Uviko-19, jambo ambalo linatishia afya za watu endapo watatumia bila kufuata ushauri wa daktari. 

Shirika la Afya Duniani (WHO) katika taarifa yake iliyotolewa April 20, 2021 linasema halishauri matumizi ya hydroxychloroquine kama tiba ya ugonjwa wa Corona kwa sababu inaweza na athari hasi kwenye moyo, figo na ini.

“Kutumia hydroxychloroquine kutibu  Uviko-19 kunaweza kusababisha mapigo ya moyo kuongezeka, matatizo ya figo na ini kushindwa kufanya kazi,” inaeleza taarifa ya WHO.

Mbali na kusababisha hatari ya magonjwa mwilini shirika hilo halipendekezi matumizi ya dawa hiyo kutokana na majaribio 30 na zaidi ya wagonjwa 10,000 yaliyofanyika kushindwa kupunguza hatari ya vifo, kulazwa hospitali kwa muda mrefu au kusaidia mfumo wa upumuaji kwa wagonjwa.

Pia wapo wanaotumia hydroxychloroquine kujikinga na maambukizi mapya ya Uviko-19, WHO inasema watu hao hawapo salama. Wanaweza kukumbwa na maudhi mengi yatokanayo na matumizi ya dawa hizo.

“Kutumia hydroxychloroquine ili kuzuia Uviko-19 kunaweza kuongeza hatari ya kuhara, kichefuchefu, maumivu ya tumbo, kusinzia na maumivu ya kichwa,” limesisitiza shirika hilo.


Soma zaidi


Hydroxychloroquine hutibu ugonjwa gani?

WHO imesema dawa ya hydroxychloroquine ni tiba sahihi ya kutibu magonjwa yanayoshambulia mfumo wa kinga ikiwemo aina ya kwanza ya kisukari na malaria na wala siyo tiba sahihi ya Uviko-19 kama inavyodhaniwa na watu wengi.

WHO wameanisha kuwa dawa ya chloroquine  ambayo hufanya kazi sawa na hydroxychloroquine kutibu magonjwa mbalimbali yaliyoainishwa na shirika hilo.

“Lakini hydroxychloroquine na chloroquine ni salama kwa matumizi kwa wagonjwa walio na magonjwa ya autoimmune (yatokanayo na kushambuliwa mfumo wa kinga) au malaria,” inasema WHO.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW