Tahadhari! ‘Ivermectin’ sio dawa ya Uviko-19

September 30, 2022 7:51 am · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni dawa ya kutibu minyoo. 
  • Hakuna dawa iliyothibitika kutibu Uviko-19 mpaka sasa.

Dar es salaam. Kumekuwako na uzushi mwingi  na taarifa potofu kuhusiana na dawa zinazoweza kutibu ugonjwa wa Uviko-19 tangu uliporipotiwa kwa mara ya kwanza mwaka 2019 huko Wuhan nchini China na kuenea maeneo tofauti duniani.

Miongoni mwa uzushi huo ni kwamba matumizi ya dawa ya ‘Ivermectin’ yanaweza kumponya mtu aliyeambukizwa Uviko-19, madai ambayo siyo ya kweli kwa mujibu wa  Shirika la Afya la Duniani (WHO).

Huu ndio ukweli

Kwa Mujibu wa WHO mpaka sasa hakuna dawa iliyothibitishwa kuwa na uwezo wa kutibu Uviko-19 hivyo madai ya dawa ya ‘Ivermectin’  kuponya ugonjwa huo si ya kweli.

Dawa ya ‘Ivermectin’ imetambuliwa na WHO kama dawa ya kutibu maradhi ya tumbo yanayosababishwa na minyoo (parasites) kwa binadamu na wanyama lakini si maalumu kwa kutibu Uviko-19.


Zinazohusiana:


Kwa mujibu wa Taasisi ya Chakula na Madawa ya nchini Marekani (FDA) wameeleza kuwa matumizi holela ya dawa hiyo yanaweza kusababisha kupata shinikizo la chini la damu, kifafa, kutapika, mzio au hata kifo.

Taasisi ya FDA pia wameonya juu ya binadamu kutumia dozi za Ivermectin zilizotengenezwa kwa ajili ya wanyama kwani huwa na uwiano mkubwa wa kemikali tofauti na zile za binadamu.

Chukua tahadhari

WHO katika taarifa yake ya mwezi Machi mwaka 2021, imeeleza katika majaribio 16 yaliyofanyika kwa watu 2,407 hayajaonesha ushahidi kuwa dawa hiyo inaweza kutibu Uviko-19.

Wimbi la taarifa potofu kipindi hiki cha janga la Uviko-19 ni kubwa kutokana na watu wengi kuchukua taarifa kutoka kwa vyanzo visivyo vya kuaminika.

WHO imetoa rai kwa watu kufuatilia taarifa za kiafya kutoka kwenye vyanzo vyake vya kuaminika ikiwemo kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Aug, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Aug, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
NISHATI

NISHATI

Nukta TV

Utani wa Rais Samia kwa wachimba madini wa Katoro

Utani wa Rais Samia kwa wachimba madini wa Katoro

Nukta TV

Rais Samia: Misaada imepungua, tukaze buti

Rais Samia: Misaada imepungua, tukaze buti

Nukta TV