Kamati yaundwa kutathmini uchumi wa vyombo vya habari Tanzania

January 24, 2023 2:13 pm · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Kamati hiyo itaangazia kwa undani hali ya uchumi katika vyombo vya habari na kutoa mapendekezo. 
  • Wadau wapongeza na kukosoa, wasema vyombo vya mtandaoni vimesahaulika.

Dar es Salaam. Huenda tasnia ya habari nchini Tanzania ikachukua sura mpya mara baada ya Serikali kuamua kulivalia njuga suala la uchumi wa vyombo vya habari pamoja na maslahi ya waandishi wa habari.

Waziri wa Habari na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye  amewaambia  wanahabari leo Januari 24, 2023 kuwa ili kutimiza hilo, Serikali imeamua kuunda kamati ya kutathmini hali ya uchumi katika vyombo vya habari.

Uamuzi huo wa Serikali unakuja wakati ambao kumekuwepo na malalamiko mbalimbali ya waandishi wa habari kuwadai waajiri wao likiwemo tukio la hivi karibuni ambapo wafanyakazi wa Sahara Media walifanya mgomo ili kudai stahiki zao.

Miongoni mwa majukumu ya kamati hiyo ambayo wanakamati wake sehemu kubwa ni wahabari ni pamoja na kupata taarifa ya hali ya vyombo vya habari kiuchumi na kiutendaji.

“Watafanya kazi ya kupata taarifa juu ya hali ya waandishi wa habari katila vyombo vya habari wakiwemo walioajiriwa, wenye mikataba, wawakilishi mikoani na wengine wanaoshirikiana na vyombo vya habari katika kupata habari, “ amesema Nape jijini Dar es Salaam.

Waziri Nape amesema kazi nyingine ya kamati hiyo ni kutathmini sababu ya changamoto za kiuchumi kwenye vyombo vya habari pamoja na kuja na mapendekezo ya kukabiliana na changamoto hizo.


Soma zaidi


Kamati hiyo itaongozwa na Tido Mhando, ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Azam Media Group huku katibu akiwa Gerson Msigwa ambaye ni Msemaji Mkuu wa Serikali ambae ataunda sekretarieti.

Wajumbe wengine wa kamati ni Dk Rose Ruben Mkurugenzi Mkuu wa Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake (Tamwa), Mkurugenzi wa vituo vya ITV na Radio One, Joyce Mwavile, na Sebastian Maganga ambaye ni Mkuu wa Maudhui wa kampuni ya Clouds Media Group.

Katika orodha hiyo ya wajumbe yupo pia Mtendaji Mkuu wa Mwananchi Communications Limited, Bakari Machumu, Kenneth Simbaya Mkurugenzi wa Shirikisho la Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania (UPTC) pamoja na Jackline Woison Mkurugenzi Mtendaji wa Multchoice Tanzania.

Kwa mujibu wa Nape kamati hiyo itafanya kazi kwa muda usiozidi miezi mitatu na kuwasilisha taarifa ili zichukuliwe hatua nyingine.

Kuundwa kwa kamati hiyo kunakutokea wakati ambao wananchi na wanahahabari wanatarajia kusikia mabadiliko yaliyofanywa na Serikali katika Sheria ya Habari ambapo kwa mujibu wa Nape yapo katika hatua za mwisho.

“Nafurahi kutoa taarifa kwamba wizarani tumekamilisha utaratibu, na tumeshawasilisha kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye atayapeleka bungeni, “ amesema Nape.

Wadau wapongeza na kukosoa

Pamoja na hatua hiyo ambayo inatarajiwa kuleta matokeo chanya kwenye tasnia ya habari, baadhi ya wadau wamekosoa kitendo cha kamati kutokuwa na mjumbe hata mmoja kutoka vyombo vya habari vya mtandaoni.

Fredrick Bundala ambaye ni Mkurugenzi xwa televisheni ya mtandaoni  ya Simulizi na Sauti, kupitia ukurasa wa Instagram ametoa maoni kwenye chapisho la Gerson Msigwa kuwa hatua hiyo ni kubwa lakini wasisahau kuangazia maslahi ya vyombo vya habari vya mtandaoni.

“Kubwa sana hii kaka, na kila la kheri katika kuyajenga. Naomba msisahau kuzungumzia online media. Bado, tunachukuliwa poa sana na makampuni. Kiuhalisia, wengi wetu tuna impact (matokeo), reach (ufikikaji)  na influence (ushawishi) kubwa sana…., “ inasomeka sehemu ya maoni hayo

Kwa upande wake mchambuzi wa masuala ya michezo nchini Edo Kumwembe kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema uhalisia unafahamika Serikali ije na suluhu.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
25 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
25 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

Nukta TV

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

Nukta TV

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

Nukta TV