Tanzania yaunga mkono azimio la chanjo kwa watoto Afrika

February 19, 2023 12:16 pm · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Azimio hilo linalenga kuimarisha huduma za chanjo kwa watoto barani humo.
  • Limepitishwa leo na wakuu wa nchi wa Umoja wa Afrika (AU).

Dar es Salaam. Tanzania imeunga mkono azimio la Umoja wa Afrika la uimarishaji wa utoaji wa huduma za chanjo kwa watoto katika nchi za Afrika baada ya mlipuko wa ugonjwa wa Uviko-19.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameunga mkono azimio hilo kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan leo Februari 19, 2023 jiji la  Addis Ababa nchini Ethiopia katika mkutano uliowahusisha wakuu wa nchi wa Umoja wa Afrika (AU).

Katika Mkutano huo imeelezwa kuwa, kufuatia janga la Uviko-19 kumekuwa na ongezeko la watoto ambao hawakupatiwa chanjo kutoka watoto milioni 7.7 mwaka 2020 hadi watoto miloni 12 mwaka 2022.

Hali hiyo imesababisha kuongezeka kwa milipuko ya magonjwa yanayoweza kuzuilika kwa chanjo ikiwemo Surua na Polio, hii ni kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani Kanda ya Africa (WHO-AFRO).

Kikao hicho kimezitaka nchi zote za Afrika kuimarisha utoaji wa chanjo kwa watoto wote ili kuhakisha magonjwa yote yanayoweza kuzuilika kwa chanjo yanamalizika.

Sambamba na hayo, kikao hicho kimetaka ajenda ya chanjo kwa watoto ibebwe na kila nchi husika na kuwa tayari kuongeza rasilimali fedha za ndani kwa ajili ya huduma za chanjo.

Waziri Ummy ameeleza kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kushirikiana na wadau wote wakiwemo sekta binafsi, hospitali binafsi, taasisi za dini, mashirika yasiyo ya kiserikali kutoa huduma za chanjo ili kuwafikia watoto wengi na hatimaye kumaliza kabisa magonjwa yote yanayoweza kuzuiliwa kwa kutumia chanjo.

Aidha, Waziri Ummy ameeleza kuwa Tanzania itatumia njia mbalimbali ikiwemo nyumba kwa nyumba ili kuwafikia watoto wote ambao hawajapata chanjo ili kuwakinga dhidi ya magonjwa mbalimbali yanayoweza zuilika kwa afua hiyo ya chanjo.

Mashirika ya kimataifa yanayohusika na utoaji wa Chanjo ikiwemo Shirika la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Shirika la Chanjo Duniani (GAVI) na WHO yameahidi kuendelea kutoa ushirikiano mkubwa kwa nchi zote za Afrika ili kuhakikisha watoto wengi wanafikiwa kwa kupata chanjo.

Pia mashirika yanayosimamia upatikanaji wa chanjo,  yameombwa kuwasimamia wazalishaji ili kuondoa tatizo la kutopatikana kwa chanjo kwenye maeneo yote.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
7 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
7 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV