Benki ya Dunia yatoa zaidi ya Sh700 bilioni kuboresha sekta ya kilimo Tanzania

June 2, 2023 8:37 am · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni kwa ajili ya programu ya kuimarisha mifumo na uhimilivu wa chakula Tanzania.
  • Unatarajiwa kuwanufaisha wakulima 300,000 moja kwa moja 

Dar es Salaam. Benki ya Dunia imeipatia Tanzania mkopo wa Dola za Marekani milioni 300, sawa na zaidi ya Sh700 bilioni kwa ajili ya kuchochea uzalishaji na kuimarisha sekta ya kilimo kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Mkopo huo umetolewa chini ya programu ya matokeo (PforR) ambayo inafadhiliwa na na Jumuiya ya Maendeleo ya Kimataifa (IDA), unalenga kusaidia utekelezaji wa programu ya kuendeleza kilimo awamu ya pili (ASDP II).

Miongoni  wa mambo yatakayotekelezwa ni pamoja na kuboresha utoaji wa huduma katika utafiti, ugani, na mbegu, kuendeleza miundombinu ya kilimo maeneo ya vijijini pamoja na kuimarisha usimamizi wa rasilimali fedha na uwekezaji.

Wakulima 300,000 sawa na asilimia 2.5 ya wakulima waliopo nchini wanatarajiwa kunufaika moja kwa moja na mkopo huo ambapo nusu yake watakuwa ni wanawake huku wengine milioni 1.8 wakinufaika kwa njia isiyo ya moja kwa moja.

Kwa mujibu wa Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, zaidi ya Watanzania milioni 12 wanajishughulisha na kilimo ambacho kinachangia asilimia 26 ya pato la Taifa na asilimia 65 ya ajira.

Hivi karibuni kumeibuka msukumo wa kuimarisha sekta ya kilimo nchini Tanzania ambapo kwa mara ya kwanza Wizara ya Kilimo imeidhinishiwa na Bunge bajeti ya Sh970.7 bilioni ambapo iliongezeka kwa asilimia 29 kulinganisha na bajeti ya mwaka 2022/23.


Soma zaidi


Nathan Belete ambaye ni Mkurugenzi wa Benki ya Dunia  nchini Tanzania amebainisha kuwa kutokana na umuhimu wa sekta ya kilimo katika ukuaji wa uchumi, mkopo huo utachochea ukuaji wa sekta hiyo pamoja na kusaidia kuimarisha uhimilivu wa chakula.

“Kilimo ni ufunguo wa ukuaji wa uchumi shirikishi na kupunguza umaskini vijijini nchini Tanzania. Programu hii itasaidia kuimarisha ukuaji wa sekta ya kilimo pamoja na mifumo himilivu ya chakula pamoja na kutengeneza ajira,” amesema Balete. 

Programu hiyo ya PforR ni awamu ya pili kati ya tatu za utekelezaji wa mradi wa kuimarisha mifumo na uhimilivu wa chakula kwa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika ambao utagharimu jumla ya  Dola milioni 903 za Marekani (zaidi ya Sh2.1 trilioni) ambapo nchi nyingine wanufaika ni pamoja na Kenya, Malawi, Somalia, Ethiopia pamoja na Madagascar.

Mabadiliko ya tabianchi, janga la Uviko-19 na vita ya Urusi na Ukraine ni miongoni mwa mambo yaliyoathiri upatikanaji wa chakula kote duniani huku nchi masikini zikiathirika zaidi.

Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, watu zaidi ya milioni 83 waliopo Kusini na Mashariki mwa Afrika wapo katika hatari ya kukabiliana na uhaba wa chakula au baa la njaa.

“Kuimarisha mifumo ya chakula, uhimilivu pamoja na kuiongezea Tanzania uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kunahitaji mabadiliko katika taasisi pamoja na namna ya kufanya kazi. Programu hiyo itakuja na njia za namna ya kukabiliana na ukame, pamoja na teknolojia za kutoa mwelekeo wa hali ya hewa,” amesema Emma Modamba mtaalam wa masuala ya uchumi na kilimo wa Benki ya Dunia.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
26 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

Nukta TV

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

Nukta TV

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

Nukta TV