Maumivu, bei ya petroli, dizeli haishikiki Tanzania

August 2, 2023 2:09 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Petroli yapaa kwa Sh463 na dizeli Sh391
  • Changamoto za upatikanaji wa Dola ya Marekani na kuporomoka kwa Shilingi vyatajwa kama sababu.

Dar es Salaam.Unaweza kusema ni maumivu juu ya maumivu kwa watumiaji wa vyombo vya moto nchini Tanzania mara baada ya bei ya mafuta ya petroli, dizeli kupaa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo changamoto za upatikanaji wa Dola za Marekani.

Kwa mujibu wa bei mpya za rejereja zilizotangazwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) zitakazo anza kutumika leo August 2, 2023 bei ya mafuta ya petroli imepanda hadi Sh3,199 kwa lita kutoka Sh2,736 iliyokuwa ikitumika mwezi Julai mwaka huu.

Hilo ni ongezeko la Sh463 kwa kila lita moja ya petroli kulinganisha na bei ya mwezi uliopita ambapo bei imeongezeka kwa asilimia 16.

Bei ya mafuta ya dizeli  inayoingia kupitia bandari ya Dar es Salaam nayo imepanda huku bei ya mafuta ya taa ikishuka kiduchu na huenda  ikaleta unafu kwa watumiaji.

Bei ya mafuta ya dizeli imepanda kutoka Sh2,544 iliyokuwa ikitumika mwezi Julai  hadi Sh2,935, ongezeko hilo ni sawa Sh391 kwa kila lita.

Mafuta ya taa yaliyokuwa yakiuzwa kwa Sh2,826 mwezi uliopita sasa yanauzwa kwa Sh 2,668 kwa kila lita.


Soma zaidi


“Mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi Agosti 2023 yanatokana na changamoto za upatikanaji wa Dola za Marekani, mabadiliko ya sera za kikodi…

Kushuka kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola ya Marekani, ongezeko la gharama za mafuta katika soko la dunia na gharama za uagizaji wa mafuta,” imesema taarifa ya Ewura iliyotolewa Agosti 1, 2023.

Kuadimika kwa Dola ya Marekani kumekuwa sehemu ya kupanda kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje ya nchi katika baadhi ya nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya ambayo inakabiliwa na mfumuko mkubwa wa bei kwa sasa.

Janga la Uviko-19 pamoja na vita inayoendelea kati ya Ukraine na Urusi vinatajwa kama sababu ya uhaba wa Dola ya Marekani ambayo ndio nguzo kuu katika biashara ya kimataifa.

Kwa mujibu wa mwenendo wa bei ya mafuta nchini Tanzania kuanzia mwezi Agosti mwaka 2022, bei ya petroli ya Sh3,199 iliyotangazwa leo ndio bei ya juu zaidi tangu ruzuku ya bilioni 100 iliyowekwa na Serikali kwenye mafuta iondolewe Mei 2023.

Mifuko kutoboka zaidi 

Bula shaka kupanda huko kwa bei za mafuta ya dizeli na petroli wamiliki wa vyombo vya moto wajiandae kutoboa mifuko yao zaidi ili kuendelea kutumia vyombo hivyo vinavyorahisisha shughuli ya usafirishaji.

Kwa Mwezi Julai  Sh10,000 ilitosha kununua lita 3.6 za mafuta ya petroli, mwezi huu pesa hiyo itanunua lita 3.1 tu za mafuta, na utalazimika kuongeza Sh1,599 kupata kiwango kile kile cha mafuta.

Kwa watumiaji wa dizeli maumivu hayatofautiani sana na wale wanaotumia petroli ambapo kwa sasa Sh10,000 inaweza kununua lita 3.4 kulinganisha na lita 3.9 zilizonunuliwa wakati bei ya dizeli ikiwa Sh2,544.

kulingana na bei hizo  mpya zilizotangazwa  sasa utahitaji Sh143,955 hadi Sh207,935 kujaza gari lako mafuta ya petroli(full tank) kwa gari lenye ujazo wa kuanzia lita 43 na 65.

Mwezi uliopita lita 43 hadi 65 za petroli ziliweza kujazwa kwa Sh117,648 hadi Sh177,840.

Bei hizo ni sawa na ongezeko la Sh26,307 kwa gari linalotumia lita 43 na Sh90,095 kwa lita 65.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Nukta TV

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

Nukta TV

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV