Ahueni, bei ya petroli,dizeli yashuka kiduchu Tanzania

December 6, 2023 7:47 am · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Petroli yashuka kwa Sh136 na dizeli kwa Sh148.
  • Ewura waeleza sababu za kushuka kwa bei ya mafuta.

Dar es Salaam. Huenda watumiaji wa wa vyombo vya moto wakashusha pumzi kidogo mara baada ya bei ya petroli na dizeli kushuka kiduchu, ikichangiwa na kupungua kwa bei ya mafuta katika soko la dunia.

Bei ya mafuta nchini imekuwa ikipanda mfululizo kuanzia mwezi Julai hali inayoacha maumivu kwa watumiaji wa vyombo vya moto nchini, na kuanza kushuka kiduchu mwezi Novemba hali iliyoleta unafuu kiduchu.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ya bei mpya za mafuta zinazoanza kutumika leo Disemba 6, 2023, lita moja ya petroli Jijini Dar es Salaam inauzwa Sh 3,138 ukilinganisha na Sh3,274  iliyokuwa ikitumika mwezi Novemba mwaka huu.

Ahueni hiyo katika bei ya mafuta ya petroli ni ya Sh136 tu ambayo ni kwa mafuta yanayoingia nchini kupitia bandari ya Dar es Salaam.

Bei ya mafuta ya dizeli nayo imeshuka kwa Sh148 kutoka Sh3,374 iliyokuwa ikitumika  mwezi Novemba hadi Sh3,226 inayoanza kutumika leo.


Soma zaidi : HESLB yawapangia mkopo wanafunzi 2,177 waliokata rufaa 2023-24


Uchambuzi zaidi wa bei hizo unaonyesha kuwa kuna ahueni kidogo kwa watumiaji wa vyombo vya moto mwezi Disemba mara baada ya pungufu huo wa bei za mafuta.

Kwa sasa Sh10,000 inaweza kununua zaidi ya lita 3 za petrolii na dizeli tofauti na awali ambapo fedha hiyo ilikuwa inanunua dizeli lita mbili na petroli lita tatu pekee.

Wakazi wa Kyerwa(Ruberwa) nado wataendelea kununua mafuta kwa bei ya juu zaidi nchini ambapo watanunua petroli kwa Sh3,396  na dizeli kwa Sh3,463 ikiwa ni bei ya juu zaidi kuliko sehemu nyingine nchini.


Soma zaidi:Idadi ya waliofariki Katesh yafika 63


Sababu za kushuka kwa bei ya mafuta zatajwa

Ewura imebainisha kuwa, kushuka kwa bei ya mafuta kwa mwezi Disemba kumechanguwa na sababu mbalimbali ikiwemo kushuka kwa bei ya mafuta katika soko la dunia 

“Mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi Disemba 2023 yanatokana na kupungua kwa bei za mafuta ghafi katika soko la dunia kwa wastani wa asilimia 8.72% na gharama za uagizaji wa mafuta kwa wastani wa asilimia 27 kwa petroli na asilimia 23 kwa dizeli,” imebainisha taarifa ya Ewura.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Nukta TV

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

Nukta TV

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV