Chanjo ya Uviko-19 inayowafaa watoto

October 30, 2021 9:45 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni aina ya Pfizer-BioNTech inayotengenezwa nchini Ujerumani.
  • Imethibitishwa kufanya kazi kwa asilimia 90.
  • Itasaidia kuepusha maambukizi ya Corona kwa watoto.

Dar es Salaam. Mamlaka ya Chakula na Dawa Marekani (FDA) imeidhinisha chanjo ya Corona (uVIKO-19) aina ya Pfizer-BioNTech kwa watoto wa miaka mitano hadi 11.

Taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo jana imesema chanjo hiyo inayotengenezwa nchini Ujerumani imepitishwa ili kuepusha maambukizi ya ugonjwa huo kwa watoto ambao awali hakukuwa na chanjo kwa ajili yao.

Mathalan, kwa Marekani pekee, asilimia 39 ya visa vya ugonjwa wa Uviko-19 kwa watoto wenye umri chini ya miaka 18 vilitoka katika kundi la watoto wa miaka mitano hadi 11.

Kati ya visa hivyo, watoto 8,300 walifikia hatua ya kulazwa na hadi mwanzoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu, watoto 146 nchini humo wameripotiwa kufariki.

Kwa mujibu wa FDA, chanjo hiyo imethibitishwa kuwa na ufanisi wa asilimia 90.7 ya kupambana na virusi vya corona.

“Kuwachanja watoto dhidi ya Corona kunatusogeza karibu  na kurejea kwenye hali ya kawaida,” amesema Kaimu Kamishna wa FDA, Dk Janet Woodcock.

FDA imesema chanjo hiyo imekidhi vigezo vyote vinavyotakiwa. tazama video hii fupi kujifunza zaidi.

                     

Makala hii imefadhiliwa na Shirika la maendeleo ya habari la International Media Support (IMS) na Umoja wa Ulaya (EU).

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
27 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
27 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
27 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wizara tano zilizoidhinishiwa fedha nyingi 2026-27

Wizara tano zilizoidhinishiwa fedha nyingi 2026-27

Nukta TV

Waziri Khamis: Serikali haijaongeza kodi kwa bodaboda

Waziri Khamis: Serikali haijaongeza kodi kwa bodaboda

Nukta TV

Nyavu za samaki zamuibua Ado Shaibu bungeni, Spika Zungu amtuliza

Nyavu za samaki zamuibua Ado Shaibu bungeni, Spika Zungu amtuliza

Nukta TV