Wanasayansi watengeneza vidonge kupunguza makali ya Uviko-19

November 6, 2021 9:25 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni vidonge vya  Paxlovid vinatengenezwa na kampuni ya Pfizer ambayo pia imetengeneza chanjo ya Corona.
  • Vimethibitishwa kupunguza vifo na wagonjwa kulazwa kwa asilimia 89.
  • Watu washauriwa kuendelea kuchukua tahadhari ikiwemo kupata chanjo.

Dar es Salaam. Kampuni ya kutengeneza dawa ya Pfizer Inc, imetangaza matokeo ya majaribio ya vidonge dhidi ya virusi vya Corona (Uviko-19) ambapo imethibitisha kuwa vidonge hivyo vinaweza kupunguza makali ya ugonjwa huo ikiwemo kumuepusha mtu kulazwa hospitalini au kifo.

Katika habari iliyotolewa na kampuni hiyo ya nchini Marekani inayotengenza pia chanjo ya Uviko-19 aina ya Pfizer-BioNTech imeeleza kuwa, vidonge hivyo vilivyopewa jina la Paxlovid vimefanyiwa majaribio kwa watu waliokuwa wakiumwa ugonjwa huo. 

Kwa mujibu wa Pfizer, katika kipindi cha majaribio, hakuna vifo vilivyoripotiwa miongoni mwa wagonjwa waliopewa vidonge hivyo ambao walionyesha dalili za ugonjwa wa Corona ndani ya siku tatu hadi tano.

Hata hivo, wagonjwa wengine ambao walipewa dawa za aina nyingine dhidi ya Uviko-19, baadhi yao walizidiwa huku wengine wakipoteza maisha.

Majaribio ya vidonge vya  Paxlovid yamefanya kwa watu wazima 1,219 ambao walipimwa na kuthibitishwa kuwa na maambukizi ya virusi vya corona.

Vidonge vya Paxlovid vimejaribiwa kwa watu zaidi ya 1,000. Picha hii siyo ya vidonge halisi. Picha| RTE.

Watu hao walikuwa wakionyesha dalili za wastani za ugonjwa huo wakiwemo wenye changamoto za afya ambazo ni hatarishi ikiwemo kisukari na matatizo ya mapafu.

Ripoti ya Pfizer inasema kuwa, dawa hiyo inafanya kazi kwa kuzuia kirusi cha corona kuzaliana ndani ya seli ambapo mgonjwa anapewa vidonge 30 ndani ya siku tano sawa na vidonge sita kwa siku.

Ripoti ya Pfizer na takwimu zitafikishwa kwenye mamlaka husika ili viruhusiwe kutumika kwa matumizi ya dharula.

shirika la Habari la The Verge limeandika kuwa, changamoto ya vidonge hivyo ni upatikanaji wake na vinatakiwa kutumika katika kipindi ambacho ugonjwa wa Uviko-19 haujakomaa ambapo ndipo vifanye kazi kwa ufanisi zaidi.

“Endapo watu hawatoweza kupata majibu ya vipimo vya corona au kuonana na daktari ndani ya muda mfupi wanapojisikia kuumwa, hawatonufaika na dawa hiyo,” imeandika The Verge.

Kamishna wa zamani wa Mamlaka ya Chakula na Dawa  nchini Marekani (FDA), Scott Gottlieb aliwahi kuliambia Shirika la Habari la CNN kuwa, “kupatikana kwa vidonge vya kuzuia kuzaliana kwa virusi ambavyo vitazuia kuzaliana kwa hiki kirusi (covid19) itakuwa ni mapinduzi.” 

Muhimu ni kufahamu kuwa dawa hizo siyo kinga ya ugonjwa huo. Watu wanashauriwa kuchanjwa chanjo ya Uviko-19 na kuendelea kuchukua tahadhari zote zinazopendekezwa na wataalam wa afya ikiwemo kuvaa barakoa.

Makala hii imefadhiliwa na Shirika la maendeleo ya habari la International Media Support (IMS) na Umoja wa Ulaya (EU).

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Nukta TV

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

Nukta TV

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV