WHO yapendekeza dawa mbili kupunguza makali ya Corona
- Dawa hizo ni “baricitinib na “monoclonal, sotrovimab”.
- Zinawafaa watu walioko hatarini kulazwa.
- Zaidi ya wagonjwa 4000 tayari wamefanyiwa majaribio.
Dar es Salaam. Shirika la Afya Duniani (WHO) imependekeza dawa mbili mpya za Corona (Uviko-19) ikiwemo ya “baricitinib” ili kutoa uchaguzi zaidi za kutibu ugonjwa huo.
WHO imesema kiwango ambacho dawa hizo zitaokoa maisha ya watu inategemea jinsi zitakavyopatikana kwa wingi na kwa bei nafuu.
Dawa ya kwanza, baricitinib, inapendekezwa kwa wagonjwa walio na Uviko-19 mkali au mbaya. Ni sehemu ya kundi la dawa zinazoitwa “Janus Kinase (JAK)” ambazo hukandamiza uchocheaji kupita kiasi wa mfumo wa kinga.
Shirika hilo linapendekeza mgonjwa apewe pamoja na dawa aina ya “corticosteroids.”
Baricitinib ni dawa ya mdomo inayotumiwa katika matibabu ya maunguo ya viungo ambapo ni mbadala kwa dawa zingine za ugonjwa huo (Interleukin-6 receptor blockers) iliyopendekezwa na WHO mnamo Julai 2021.
WHO pia imependekeza kwa masharti matumizi ya dawa ya kingamwili ya “monoclonal, sotrovimab”, kwa ajili ya kutibu Uviko-19 wa wastani au kwa wagonjwa walio katika hatari kubwa ya kulazwa hospitalini.
Hii ni pamoja na wagonjwa ambao ni wazee, wasio na kinga, walio na magonjwa sugu kama vile kisukari, shinikizo la damu, na unene uliokithiri, na wale ambao hawajachanjwa.
Sotrovimab ni mbadala wa dawa ya “casirivimab-imdevimab” iliyopendekezwa na WHO Septemba 2021.
Zinazohusiana.
- Picha za tetemeko Croatia zilivyotumika kupotosha Corona mtandaoni
- Siyo kweli wananchi Italia wanatupa pesa mitaani kuepuka Corona
Uchunguzi unaendelea kuhusu ufanisi wa dawa hizo dhidi ya Omicron lakini tafiti za awali za maabara zinaonyesha kuwa sotrovimab ina uwezo mkubwa wa kupunguza makali ya kirusi hicho.
Jopo la wataalam wanaounda miongozo hiyo pia waliangalia dawa zingine mbili za Uviko-19 kali na muhimu: ruxolitinib na tofacitinib. Kwa kuzingatia athari zao zisizo na uhakika, WHO ilitoa pendekezo la masharti dhidi ya matumizi yao.
Mapendekezo hayo, yanayounda sasisho la nane la miongozo ya WHO juu ya matibabu na Uviko-19, yanatokana na ushahidi kutoka kwa majaribio saba yanayohusisha zaidi ya wagonjwa 4,000 walio na ugonjwa huo usio mkali.
WHO iko kwenye majadiliano na watengenezaji wa dawa ili kuhakikisha dawa hizo zinasambazwa duniani kote hasa katika nchi zenye kipato cha chini ili kuwapunguzia watu maumivu ya Uviko-19.
Mbali na hatua hiyo, WHO pia ipo mbioni katika kuhakikisha chanjo inatolewa kwa watu wote ambapo kwa barani Afrika mwitikio bado ni hafifu takribani aslimia 85 ya watu bado hawajachanja kwa mujibu wa shirika hilo.
Latest
