Jinsi ya kuhamisha “chati” za WhatsApp kutoka simu za Android kwenda iPhone

January 24, 2022 1:29 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Whatsapp inatarajia kuachilia huduma hiyo hivi karibuni.
  • Itarahisisha watumiaji wa Android kubaki na chat zao hata wanapohamia IOS.
  • Mfumo huo utaambatana na sasisho la WhatsApp kwenye IOS la hivi karibuni.

Dar es Salaam. Kila mara unaposasisha simu kutoka kutumia simu za android kwenda simu za IOS, ni kama unaanza maisha upya. Mbali na kupoteza baadhi ya kumbukumbu kama picha na taarifa za apps, unaweza kupoteza mazungumzo yako na uwapendao.

Utapoteza kumbukumbu zako ikiwemo chati ambazo ulikuwa nazo kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii kama WhatsApp na meseji za kawaida. Kwa mitandao mingine kama Instagram na Telegram, walau una uhakika wa kukuta chati zako popote utakapohamia.

Hata  hivyo, henda siku za usoni, hiyo isiwe changamoto tena kwani tayari wabunifu wapo kazini. Wabunifu kutoka mtandao wa WhatsApp wapo mbioni kuzindua mfumo ambao utawawezesha watumiaji wa simu za Android kuhama na “chat” zao pale wanapobadilisha simu na kuanza kutumia simu zenye mfumo endeshi wa iOS ambazo ni iPhone.

Tovuti ya masuala ya kiteknolojia, Andorid Central imesema mabadiliko hayo tayari yanaonekana kwenye app ya WhatsApp Messenger beta for iOS ambayo ni app ya majaribio inayotarajiwa kusasisha toleo linalotumika sasa.

Android Central imeeleza kuwa, mwaka jana WhatsApp ilikuwa ikizungumza na Apple pamoja na Google ili kuruhusu watumiaji wa simu zao kuweza kuhama na chati zao pale wanapobadilisha simu.

Mfumo huo unafanya kazi kwenye simu zote yaani kutoka Android kwenda IOS na IOS kwenda Android.


Soma zaidi:


Kati ya vitu vya kuzingatia ni pamoja na kuhakikisha kuwa simu zote yaani inayohamisha na inayohamishiwa zina chaji walau asilimia 80.

Pia ni muhimu kufahamu kuwa, endapo utaruka (skip) hatua ya kuhamisha chati hizo, hautoweza kufanya tena jambo hilo. 

Mfumo huu utaanza kufanya kazi pale WhatsApp itakapoingiza sasisho hilo kwenye maduka ya programu za Apple ya App Store.

Ili kujua hatua kwa hatua ya jinsi ya kuhamisha chati kutoka simu ya Android kwenda IOS, endelea kusoma www.nukta.co.tz.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV