Guterres: Dunia inahitaji wanawake zaidi wanaokuza akili bandia

February 12, 2022 6:49 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Asema wanawake wana mchango mkubwa katika sayansi.
  • Asisitiza wapewe nafasi kuonyesha uwezo wao.
  • Akemea ubaguzi katika sayansi.

Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya viwango vya chini vya wanawake wanaofanya kazi katika masuala ya akili bandia (AI) na kanuni za upendeleo wa kijinsia ambazo huchukulia wanaume kama watu wa viwango na wanawake kama tu ilimradi.

Amesisitiza kuwa dunia inahitaji wanawake zaidi wanaokuza akili bandia ambayo inamuhudumia kila mtu na kufanya kazi kwa usawa wa kijinsia na kwamba inahitaji pia kubadilisha mienendo ambayo inawazuia wanasayansi wanawake wachanga kusoma taaluma ambazo hutusaidia kushughulikia majanga ya tabianchi na mazingira. 

“Nilifundisha uhandisi. Ninajua kutokana na uzoefu binafsi kwamba wasichana na wanaume wana uwezo sawa na wanavutiwa sawa na sayansi, iliyojaa mawazo, na wako tayari kuendeleza ulimwengu wetu mbele,” amesema.   

Amesema ni lazima dunia ihakikishe wanawake wanapata fursa sawa za kujifunza na kufanya kazi kwenye uwanja sawa hasa kuendeleza teknolojia ya AI. 

“Katika Siku hii ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi, ninatoa wito kwa kila mtu kuunda mazingira ambapo wanawake wanaweza kutambua uwezo wao wa kweli na wasichana wa leo wanakuwa wanasayansi na wavumbuzi wakuu wa kesho, wakiunda mustakabali mzuri na endelevu kwa wote,” amesema Guterres.

Ametoa kauli hiyo kupitia katika ujumbe wake wa Siku Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Wayansi iliyoadhimishwa Februari 11 akisema kuwa hivi sasa ni mtu 1 tu kati ya watafiti 3 wa sayansi na uhandisi ulimwenguni ambaye ni mwanamke.

Amesema vikwazo vya kimuundo na kijamii vinazuia wanawake na wasichana kuingia na kuendelea katika sayansi. 


Zinazohusiana:


Pia Janga la Uviko-19 limeongeza zaidi ukosefu wa usawa wa kijinsia, kuanzia kwenye kufungwa kwa shule hadi kuongezeka kwa vurugu na mzigo mkubwa wa huduma nyumbani. 

“Ukosefu huu wa usawa unanyima ulimwengu wetu vipaji na ubunifu mkubwa ambao haujatumiwa. Tunahitaji mitazamo ya wanawake ili kuhakikisha sayansi na teknolojia inafanya kazi kwa kila mtu,” amesema Guterres.

Aidha Guterres ameshauri hatua ambazo anaona ni muhimu kuzichukua akisema ulimwengu unaweza na ni lazima kuchukua hatua kwa kuwa na sera zinazojaza madarasa na wasichana wanaosoma teknolojia, fizikia, uhandisi, hesabu. 

Hilo linatakiwa liende sambamba na hatua zinazolenga kuhakikisha fursa za wanawake kukua na kuongoza katika maabara, taasisi za utafiti na vyuo vikuu. 

Dhamira ya kukomesha ubaguzi na mila potofu kuhusu wanawake katika sayansi na kupanua fursa kwa wanawake wa jamii za watu wachache.  

“Haya yote ni muhimu katika uwanja muhimu wa akili bandia.” amesisitiza. 

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
25 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
25 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

Nukta TV

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

Nukta TV

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

Nukta TV