Zaidi ya Sh11 trilioni kulipa deni la Serikali mwaka 2022-23

March 12, 2022 10:26 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Fedha hizo ni asilimia 27.5 ya bajeti ya mwaka 2022/23.
  • Serikali inakusidia kutumia bajeti ya Sh41.1 trilioni mwaka ujao.

Dar es Salaam. Waziri wa Fedha na Mipango Dk Mwigulu Nchemba  amesema katika mwaka wa fedha wa 2022/2023 inakadiria kutumia bajeti ya Sh41.1 trilioni huku zaidi ya robo ya fedha hizo zitatumika kulipa deni la Serikali. 

Dk Nchemba katika hotuba yake ya mapendekezo ya ukomo wa bajeti ya Serikali kwa mwaka 2022/23 ya Machi 11, 2022, Bungeni jijini Dodoma amesema bajeti hiyo ni ongezeko la asilimia 8.1 ikilinganishwa na makadirio ya mwaka 2021/22 ya Sh37.9 trilioni.

Kati ya kiasi hicho kitakachotumika mwaka ujao, Sh25.5 trilioni zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida ikiwa ni asilimia 62.2 ya bajeti yote, ikijumuisha Sh11.3 trilioni kwa ajili ya ulipaji wa deni la Serikali.

Kiasi hicho cha fedha kilichotengwa kwa ajili ya kulipa deni ni sawa na asilimia 27.5 au juu kidogo ya robo ya bajeti yote.

Pia matumizi ya maendeleo yanatarajiwa kuwa Sh15.5 trilioni, sawa na asilimia 37.8 ya bajeti yote.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
21 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
21 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Nukta TV

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Nukta TV

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

Nukta TV