Majaliwa aingilia kati kupanda bei za bidhaa Tanzania

April 23, 2022 6:09 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wananchi kwamba bidhaa nyingi zimepanda bei.
  • Ataka waliopandisha kiholela wachukuliwe hatua.

Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wafanye ziara kwenye masoko na maduka ili kupata hali halisi ya bei za bidhaa na wachukue hatua kudhibiti upandaji holela wa bei hizo. 

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo Aprili 22, 2022 wakati akizungumza na viongozi wa mikoa na wilaya kuhusu maendeleo ya maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi kwenye kikao kazi alichokiendesha kwa njia ya mitandao (video conference) kutokea ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma.

“Tumepata malalamiko kutoka kwa wananchi kwamba bidhaa nyingi zimepanda bei, ninyi ni Wenyeviti wa Kamati za Bei na Kamati za Kodi kwenye mikoa na wilaya zenu. Upandaji wa bei sasa umekuwa holela. Ni jukumu lenu kufanya ufuatiliaji wa bei za mazo katika masoko yenu,” amesema Majaliwa.

Waziri Mkuu amesema ziko bidhaa ambazo zinazalishwa nchini kama vile nondo au saruji ambazo hazipaswi kupanda bei hasa baada ya kutolewa tamko na Waziri wa Fedha na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara kwamba wameshaongea na wenye viwanda na wakakubaliana kuwa bidhaa zote za ndani zinapata nafuu ya kodi.

“Sasa iweje hali iendelee kuwa vilevile?”, amehoji na kuongeza: “Vyakula vinavyozalishwa nchini kama mchele, Shinyanga mchele mwingi, Tabora mchele mwingi, Mbeya nako mchele mwingi kuna sababu gani ya kupadisha mchele wakati unazalishwa nchini?,” amehoji Majaliwa.

                   

“Ninawaagiza, fanyeni ziara kwenye masoko yenu, fanyeni tafiti na mtathmini ni kwa nini bei zinapanda. Mchicha unapandaje bei, ni kwa sababu ya nini? Zungumzeni na tuone mkianza kudhibiti hiyo hali. Na Kama kuna maeneo bei inapanda kiholela, hakikisheni bei inashuka iende kwenye bei halisi ili tuwasaidie wananchi,” amesema Waziri Mkuu. 

/
No matches found for this filter
31 May, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
31 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
31 May, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

Nukta TV

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

Nukta TV

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

Nukta TV