Uviko-19: Kutopata mabadiliko baada ya kuchanjwa haimaanishi umepata chanjo feki

October 7, 2022 11:59 am · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Wataalamu wasisitiza mabadiliko hutokea kwa namna tofauti kulingana na mhusika.

Dar es salaam. Chanjo ya Uviko-19 inaendelea kutolewa na mataifa mbalimbali duniani kama njia mojawapo ya kupambana na ugonjwa huo ambao umeathiri pakubwa shughuli za kijamii na kiuchumi duniani.

Siku za hivi karibuni kumeripotiwa kuwepo kwa uzushi kuwa wale ambao hawakupata mabadiliko ya kimwili mara baada ya kupata chanjo basi hawakuchanjwa chanjo halisi ya Uviko-19 bali ‘placebo’.

WHO kanda ya Afrika  katika taarifa yake iliyochapishwa Septemba 29 kwa mfumo wa video katika mtandao wa Twitter imekanusha uzushi huo na kueleza kuwa ‘placebo’ hutumika tu wakati wa majaribio ya dawa au chanjo na hufanyika maabara pekee.


Soma zaidi:


Placebo ni nini

WHO imeeleza kuwa placebo ni dutu ambazo hutumika wakati wa kufanya majaribio ya dawa maabara. Husajiliwa na kufanana na dawa lakini hazina kemikali hai ndani yake.

“Dutu hizi hutumika maabara pekee chini ya uangalizi maalum na haziruhusiwi kutumika nje ya maabara,” inafafanua sehemu ya taarifa ya WHO.

Kutopata mabadiliko ya kimwili mara baada ya kupokea chanjo ya Uviko-19 haimaanishi kuwa umepokea chanjo feki au chanjo haifanyi kazi bali mabadiliko yanakuwa yanatokea katika namna nyingine.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya ulimwenguni WHO hadi Octoba 6,2022 jumla ya chanjo bilioni 12.7 zimetolewa duniani kote huku watu bilioni 5.3 wakipata angalau dozi moja ya chanjo na watu bilioni 4.9 wakipata dozi kamili ya chanjo.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
25 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
25 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

Nukta TV

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

Nukta TV

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

Nukta TV