Apple yasogeza mbele uzinduzi wa toleo jipya iPad

August 4, 2022 1:42 pm · Davis Matambo
Share
Tweet
Copy Link
  • Itazindua Oktoba badala ya Septemba.
  • Lengo ni kupata muda wa kuboresha zaidi mfumo huo.

Watumiaji wa bidhaa za Apple ya Marekani watalazimika kusubiri hadi Oktoba mwaka huu wakati kampuni hiyo ikiboresha toleo jipya la tableti zake.

Awali Apple inayotengeneza simu aina ya iPhone ilipanga kufanya uzinduzi huo Sepetemba 2022 lakini imesema bado haijakamilisha taratibu za kuuboresha mfumo wa endeshi (IPadOS) katika tableti hizo.

Imesema inahitaji muda wa kutosha kufanya maboresho yatakoyoziwezesha tableti mpya kuwa na ufanisi wa kufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja.

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Bloomberg, Apple inafanyia kazi kipengele kipya cha “stage manager” kilichopo kwenye tableti hizo.


Zinazohusiana;


Kipengele hicho kitaruhusu watumiaji kuvinjari kwa urahisi na haraka wakati wanatumia kifaa hicho cha mawasiliano.

Kawaida kampuni hiyo hutoa mifumo mipya ya uendeshaji wa iPhone na iPad kwa wakati mmoja Septemba kila mwaka.

Hii ina maana kuwa iPadOS 16 haitatoka hadi Oktoba, mwezi mmoja baada ya kutolewa kwa mfumo mpya endeshi  wa iPhone.

Inajumuisha ‘sasisho kubwa zaidi kuwahi kutokea’ kwa skrini iliyofungwa, ambayo hurahisisha kubadilisha picha za mandharinyuma na rangi na muundo wa fonti za onyesho.

/
No matches found for this filter
26 May, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
26 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: KOMBO AKIWASILISHA BAJETI YA WIZARA YA MAMBO YA NJE BUNGENI 2026/2027

🔴LIVE: KOMBO AKIWASILISHA BAJETI YA WIZARA YA MAMBO YA NJE BUNGENI 2026/2027

Nukta TV

JINSI WAHAMIAJI HARAMU WANAVYOONGEZEKA TANZANIA

JINSI WAHAMIAJI HARAMU WANAVYOONGEZEKA TANZANIA

Nukta TV

VIJANA WA TANZANIA KUNUFAIKA NA UCHUMI WA KIDIGITALI

VIJANA WA TANZANIA KUNUFAIKA NA UCHUMI WA KIDIGITALI

Nukta TV