Microsoft, Apple zawarahisishia maisha watumiaji wake

October 14, 2022 7:45 am · Davis Matambo
Share
Tweet
Copy Link
  • Zaunganisha huduma ya kuhifadhi picha, video mtandaoni.
  • Programu ya iCloud ya Apple kuwezesha watumiaji wa microsoft kupata picha kwa urahisi.  

Dar es Salaam. Watumiaji wa Microsoft wanaotumia mfumo endeshi wa Windows 11 hawatakua na hofu tena ya kuzipata picha zao kwenye simu za iPhone na tableti za iPad kwa sababu suluhu imepatikana.

Wataweza kuzipata kwa sababu kampuni ya Microsoft ya Marekani imeunganisha programu yake na huduma ya iCloud ya kampuni ya Apple inayotumika kuhifadhi vitu mtandaoni.

Maboresho haya yanayolenga uunganishaji wa huduma za kampuni hizi mbili  yametangazwa kwenye blogu ya Microsoft katika tukio maalum la Microsoft’s Surface la Oktoba 12, 2022 wakati kampuni ya Redmond ilipokuwa ikitambulisha vifaa vyake vipya.

Uunganishi huu wa huduma utawawezesha watumiaji wa vifaa vya Apple kufungua video na picha zao kwa kutumia kompyuta za Microsoft kwa kutumia huduma ya uhifadhi wa mtandaoni ya iCloud.

iCloud ni huduma kutoka Apple ambayo inawezesha uhifadhi na ushiriki wa picha, mafaili, madokezo, nenosiri na data nyingine kwa usalama kupitia mtandao na kuzisasisha kiotomatiki kwenye vifaa vyote kwa watumiaji wake.

“Programu ya Picha za Microsoft hukuruhusu kuona, kupanga, na kushiriki picha kutoka OneDrive kwenye Kompyuta yako, na ukiwa na sasisho hili, utaweza kuongeza na kufikia picha zako za iCloud moja kwa moja kutoka ndani ya programu pia,” Dave Grochocki, Meneja Mkuu wa Bidhaa kutoka Microsoft amesema.


Soma zaidi

Ili kufanikisha uunganishaji huu, mtumiaji anapaswa kupakua programu ya iCloud kupitia duka la Microsoft store kisha kuingia kwa kutumia utambulisho wake wa Apple (Apple ID).

Kumbuka kuchagua kipengele cha Picha cha ndani ya program ili kuiruhusu Microsoft 11 kufuingua maktaba ya iCloud.

Kwa sasa, programu hii mpya ya picha (iCloud Photos) inapatikana kwenye Dev Channel kwa baadhi ya watumiaji wa Microsoft Windows Insider, lakini itapatikana kwa watumiaji wote kufikia Novemba mwaka huu.

Uunganishaji wa programu za kampuni za Microsoft na Apple unawapa watumiaji wao uwezo wa kuzifikia na kufungua picha, muziki na vipindi vya televisheni kati ya majukwaa hayo kupitia mtandao kwa urahisi.

Huo ni mwanzo wa makampuni hayo kuongeza ushirikiano. Microsoft pia imethibisha itaachia programu za utazamaji wa vipindi vya video na muziki za watumiaji wa Apple Tv na Apple Music mapema mwaka ujao kupitia duka lake kama ilivyo kawaida.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Nukta TV

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Nukta TV