Watu zaidi ya milioni 1 kupata chanjo ya Uviko-19 Mwanza

August 25, 2022 12:50 pm · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Lengo likifanikiwa litasaidia kuongeza kinga kwa wananchi.
  • Malengo ya Tanzania ni kuchanja watu milioni 21.5 ifikapo Disemba 2022.
  • Elimu ya chanjo kuwafikia zaidi wananchi.

Mwanza. Mkoa wa Mwanza unakusudia kutoa chanjo ya Uviko-19 kwa watu 1.2 milioni ifikapo mwezi Desemba mwaka huu ili kuwakinga dhidi ya ugonjwa huo ambao umekuwa ukiisumbua dunia.

Ikiwa mkoa huo utafanikiwa kuchanja watu hao, utasaidia kufikia malengo ya Tanzania ya kuchanja watu milioni 21.5 ifikapo Disemba 2022.

Mratibu wa chanjo Mkoa wa Mwanza, Amos Kiteleja aliyekuwa akizungumza hivi karibuni na Nukta Fakti amesema katika awamu ya kwanza utoaji wa chanjo hiyo iliyofanyika katika vituo 355 jumla ya watu 479,094 walichanja angalau dozi moja.

Amesema katika awamu ya pili iliyoanza Julai hadi Desemba mwaka huu wanatarajia kuchanja zaidi ya watu 1.2 milioni sawa na asilimia 70.

“Wakati tunaanza kutoa chanjo hali haikuwa nzuri mwitikio ulikuwa mdogo, lakini baada ya elimu kutolewa mwitikio wa watu uliongezeka, na sasa tunaingia awamu ya pili ambapo tunatarajia kuchanja watu wengi zaidi,” amesema Kiteleja.

Amesema katika awamu ya pili, vituo vya kutolea chanjo vimeongezeka na kuwa elimu inazidi kutolewa kwa wananchi ikiwemo kutumia vyombo vya habari, mikutano ya hadhara na semina mbalimbali.

Amesema katika awamu hii ya utoaji wa chanjo wanalenga angalau wananchi waliopata chanjo dozi moja ya awali waongeze ziwe mbili huku wale ambao hawakupata wakipewa kipaumbele.

“Wale ambao hawajahi kupata chanjo ya Uviko-19 watapewa kipaumbele zaidi kwenye awamu hii kwa kuwa takwimu zinaonyesha kuwa wanaopata maambukizi ya Uviko-19 wengi wao ni wale ambao hawajachanja,” amesema Kiteleja.

Wananchi wanasemaje?

Nukta Fakti pia imezungumza na baadhi ya wakazi jijini Mwanza ambao wamewahi kupata chanjo ya Uviko-19 na kueleza kuwa wakati chanjo inaanza kutolewa walikuwa na hofu lakini baada ya kupewa elimu waliamua kuchukua hatua na kwenda kupata chanjo.

Mkazi wa Mtaa wa Nyakato jijini hapa, Transisi Balizukwa amesema wananchi hawapaswi kuendelea kuwa na hofu tena kwani chanjo kama hizo ziliwahi kutolewa tena miaka ya nyuma mathalani chanjo ya kifua kikuu, polio na surua.

“Ukweli wazee tulikuwa na hofu baada ya Corona kuingia nchini na baada ya kupatikana kwa chanjo  ya ugonjwa huo hofu imeondoka  ikizingatiwa hadi sasa hatujasikia mtu aliyepata madhara kutokana na chanjo hiyo hivyo wito kwa wazee na jamii ikubali kuchanjwa chanjo hiyo ya uviko-19,” amesema Balizukwa.

Amina Said mkazi wa Buzuruga amesema amepata chanjo ya Uviko-19 na hakupata shida yoyote kwenye mwili wake na kuwashauri wazee wakubaliane na suala hilo ili kuepuka maradhi yanayosababishwa na ugonjwa huo.

“Jamii inapaswa kujua kuwa toka Serikali ianze kutoa chanjo ya Uviko-19 hatujasikia kuwa mtu amechanjwa na amekufa hivyo ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha kuwa anapata chanjo ya uviko ili kujikinga,” amesema Amina.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya, hadi kufikia Julai 29 mwaka watu milioni 4.22 walikuwa wamepata chanjo ya Uviko-19 ikiwa ni pungufu ya mara tano ya lengo lililowekwa la watu milioni 21.5 ifikapo Decemba mwaka huu.

Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Mohamed Yusuph amesema wapo baadhi ya wananchi wanachukulia suala hili kimila na wanapoenda kuchanja wanaenda kwa kujificha wakihofia kuwa familia itamtenga.

“Pamoja na hamasa inayotolewa lakini bado kuna familia zimeshikilia misimamo ya kimila kitendo hicho ni hatari kwa kuwa wanahatarisha maisha yao,” amesema Yusuph.

/
No matches found for this filter
26 May, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
26 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

Nukta TV

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

Nukta TV

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

Nukta TV