Majaliwa aungana na viongozi wa dunia kumuaga Shinzo Abe

September 27, 2022 1:26 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary leo Septemba 27, 2022 wameshiriki katika mazishi ya kitaifa ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo  Abe yaliyofanyika Tokyo nchini Japan. Picha | Ofisi ya Waziri Mkuu.


  • Ni aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Japan.

Dar es Salaam. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameungana na viongozi mbalimbali duniani kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Waziri Mkuu mstaafu wa Japan, Shinzo Abe akimuwakilisha Rais Ramia Suluhu Hassan.

Waziri Majaliwa ameungana na wakuu wa nchi na viongozi 700 kutoka nchi 195 na mashirika ya kimataifa 23, kwenye mazishi ya kiongozi huyo yaliyofanyika katika ukumbi wa Nippon Budokan jijini Tokyo nchini Japan, 

Baadaye alizuru kasri la kifalme la Akasaka  ili kuwapa pole wafiwa.

Waziri Majaliwa akiwa miongoni mwa viongozi 40 ulimwenguni, ameonana na kumfariji Waziri mkuu wa sasa wa Japan Fumio Kishida kisha kumpa pole mjane wa Hayati Shinzo Abe, Akie Abe.

Majaliwa aliambatana na mkewe Mary Majaliwa, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk, Balozi wa Tanzania nchini Japan, Balozi Baraka Luvanda na mkewe Consolata Luvanda.

Viongozi wengine walioshiriki mazishi hayo ni Marais kutoka Vietnam, Marekani, Ufilipino, Rais Mstaafu wa Ufaransa, Ujerumani na Mfalme wa Falme za Kiarabu, Makamu wa Rais kutoka Indonesia, Mtawala wa Qatar na Amiri wa Kuwait na Mawaziri Wakuu 16 kutoka mataifa mbalimbali ulimwenguni .

Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Ofisi ya Waziri Mkuu wa Tanzania, imeosha kuwa Zaidi ya watu 4,300 walikuwa ukumbini kuaga mwili wa kiongozi Shinzo Abe, huku mapema asubuhi ya leo wakazi wa Japani walijipanga misururu kutoa salamu za mwisho kwa kuweka mashada ya maua kwenye eneo maalumu lililoandaliwa kumuaga kiongozi huyo.

Hayati Shinzo Abe alizaliwa Septemba 21, 1954 na amehudumu kama Waziri Mkuu wa Japan na Rais wa chama cha Liberal Democratic Party (LDP) kutoka mwaka 2006 hadi 2007.

Alishika wadhifa huo tena kutoka mwaka 2012 hadi 2020 na kufariki Julai 8, 2022 akiwa na umri wa miaka 67.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Nukta TV

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Nukta TV