Waziri Ummy: Kuna tishio la Ebola kuingia Tanzania

September 28, 2022 11:54 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Serikali yasema mikoa 5 ikiwemo Mwanza na Kagera iko hatarini zaidi kupata ugonjwa huo.
  • Mpaka sasa hakuna hata mgonjwa mmoja aliyegundulika.
  • Wananchi watakiwa kuchukua tahadhari, Serikali  ikiendelea kuchukua hatua za kudhibiti ugonjwa huo usiingie nchini. 

Dar es Salaam. Baada ya ugonjwa wa Ebola kuishambulia Uganda, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema wananchi wachukue tahadhari kwa sababu kwa sasa kuna tishio la ugonjwa huo kuingia Tanzania.

Ummy aliyekuwa akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 28, 2022 jijini Dodoma amesema ugonjwa huo ni tishio ukizingatia ukaribu uliopo kati ya Uganda na Tanzania.

“Kwa hiyo tumeona kutoka Mubende (Uganda) hadi kufika mpakani kwetu Mtukula mkoani Kagera kupitia Masaka  ni takribani kilometa 230 kwa hiyo mtaona siyo mbali,” amesema Waziri.

Hata hivyo, mpaka sasa hakuna mgonjwa hata mmoja aliyegundulika kupata maambukizi ya ugonjwa huo nchini.

Ugonjwa huo ni miongoni mwa magonjwa yanayosambaa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu kwa kula au kugusa mnyama mwenye maambukizi kama nyani, kima, popo na swala.

“Ugonjwa wa Ebola unaenea kutoka kwa binadamu mmoja kwenda kwa mwingine kwa kugusa majimaji ya mwili wa mgonjwa kwa mfano mate, machozi, damu, matapishi, mkojo na kinyesi. Endapo mtu ataona dalili hizi awahi kituo cha kutolea huduma za afya,” amesisitiza Waziri Ummy.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya Uganda, hadi kufikia Septemba 25 mwaka huu watu 36 walikuwa wameugua ugonjwa huo ambapo 23 kati yao wamefariki dunia.


Zinazohusiana:



Mikoa iliyo katika hatari zaidi

Waziri Ummy ameitaja mikoa mitano ambayo iko katika hatari zaidi ya kupata ugonjwa huo kuwa ni Kagera, Mwanza, Kigoma, Geita na Mara 

Mikoa iliyo katika hatari ya kati ni pamoja na Dar es Salaam, Kilimanjaro, Songwe, Dodoma na Arusha kutokana kuwa na viwanja vya ndege ambavyo vinapokea wageni wa kimataifa.


Serikali inachukua hatua gani?

Kufutia mlipuko wa ugonjwa huo nchini Uganda, Serikali ya Tanzania imejipanga kufanya taratibu mbalimbali kuhakikisha ugonjwa huu hauingii nchini ikiwemo kutoa elimu, kutoa vifaa tiba na dawa za kutosha.

Serikali pia imeandaaa dawa na vifaa tiba muhimu vinavyotakiwa kuwepo kwenye vituo vya afya hususani  kwenye mikoa iliyopo hatarini zaidi ikiwemo mkoa wa Kagera.

“Tunahakikisha kwamba endapo watapata mgonjwa basi wanafanya kazi zao za kutoa huduma ambayo ni salama kwao na kwa mgonjwa,“ amesema Ummy.

Pia Serikali itaimarisha uchunguzi kwenye mipaka yenye  muingiliano mkubwa na nchi zenye maambukizi ya ugonjwa huo.

“Kuimarisha ufuatiliaji wa tetesi za watu wenye viashiria vya ugonjwa kwenye jamii na vituo vya kutolea huduma na kuwahudumia wagonjwa watakao thibitika, kuimarisha mfumo wa usafirishaji wa sampuli kwa ajili ya kufikisha maabara ya Taifa,” amesema Ummy.

Aidha, Waziri huyo amewataka wananchi kuchukua tahadhari kuhakikisha ugonjwa huu hauingii nchini Tanzania .

“Mimi bado naaamini kabisa Watanzania tuna uwezo wa kuhakikisha ugonjwa huu hauingii nchi,” amesema Waziri Ummy.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV