Fanya haya kuboresha ulaji wa chakula

Joshua Sultan 0458Hrs   Oktoba 05, 2019 Maoni & Uchambuzi
  • Maisha ya mwanadamu ni mtiririko wa kanuni moja hadi nyingine, hata ulaji wa chakula una kanuni zake.
  • Zingatia kuwa na mpangilio katika ratiba yako ya kula, uwe na kiasi na epuka mchanganyiko wa vyakula vingi kwa wakati mmoja.

Maisha ya mwanadamu ni mtiririko wa kanuni moja hadi nyingine. Tangu unazaliwa mpaka hatua uliyofikia, kuna kanuni kadha wa kadha ambazo umezipitia mpaka sasa. 

Hata shuleni, kuna na utitiri wa kanuni nyingi hasa katika masomo ya sayansi. Mojawapo ya kanuni rahisi ya ngazi za chini ni ile ya “nenda na moja kichwani” katika hisabati za kujumlisha. 

Siku moja nikiwa napitia mtandaoni nikakutana na bandiko (Post) watu wakiuliza baadhi ya kanuni “konki” walizotumia shuleni lakini mpaka wanakuwa watu wazima hwajaona kabisa walipopata kuzitumia. 

Hivyo hivyo, katika afya kuna kanuni nyingi za kuzingatia. Kuna hiki cha kuacha, usifanye hiki, zingatia kile na kadhalika. Ni dhahiri kuwa kanuni hizi kwa baadhi ya watu niliowahi kukaa nao huniambia kwa Kiswahili cha kisasa “zinaboa” na zinaleta ukakasi wa kuzifautilia wakati mwingine. 

Leo nataka tuone kanuni kadhaa rahisi sana ambazo unaweza kuzizingatia kwa ajili ya kuimarisha na kulinda afya yako.

Weka ratiba inayoeleweka ya chakula

Zingatia kuwa na mpangilio katika ratiba yako ya kula. Usile mapema sana wala ukiwa umechelewa sana, ila jitahidi kuwa na ratiba yenye mpangilio katika namna unavyokula. 

Tumbo lako limezoea kula kwa wakati fulani kila siku. Mfano kama unapata chai saa tatu asubuhi, chakula chako cha mchana saa nane na chakula cha usiku saa mbili usiku kila siku. Ni vyema kuzingatia mpangilio huu kila siku.

Hivyo hivyo, katika afya kuna kanuni nyingi za kuzingatia. Kuna hiki cha kuacha, usifanye hiki, zingatia kile na kadhalika. Picha|Mtandao.

Kuwa na kiasi  

Ni vizuri kuwa na kiasi kwa kila kitu unachofanya. Hata katika ulaji wako ni vizuri kuwa na kiasi unapokula. Kula kwa kiasi unachohitaji tu. Usile kupita kiasi. Kula kuridhisha njaa yako kisha acha.

Kula kwa mabonge madogo (take small bites). Weka kiasi kidogo cha chakula ndani ya kinywa chako kwa hatua. Hii husaidia kukitafuna ipasavyo na kuyeyusha ipasavyo kwa kemikali zilizo ndani ya kinywa chako. 

Kula taratibu

Tulia (relax) na kula taratibu, usikimbizane na mtu. Kama una haraka ni vyema kuacha kula kwa wakati huo. Usiwe na haraka, msongo, hofu, uchovu au hasira wakati wa kula. Tafuna chakula chako vizuri unapokula. Usile vitu vingi kwa wakati mmoja katika mlo mmoja. 


Zinazohusiana:


Epuka kuchanganya vitu vingi katika mlo wako

Pia vionjo vingi kwenye chakula kupita kiasi mara nyingi hulivuruga tumbo. Pangilia milo yako kutoka mlo mmoja hadi mwingine kwa kuwa na vitu tofauti tofauti. 

Kama ulikula ngano asubuhi, unaweza jaribu kitu kingine jioni kama mchele au unga wa muhogo. Epuka mchanganyiko wa vyakula vya aina nyingi kwa wakati mmoja. 

Inashauriwa kuepuka kula vyakula au vilivyoandaliwa kwenye vyombo vyenye aluminiamu nyingi. Pia vinywaji vilivyo ndani ya vyombo vya aluminiamu siyo vizuri. 

Aluminiamu inahusishwa kwa ukaribu sana na magonjwa ya kupoteza kumbukumbu ( Alzheimer’s disease). Pia ni vyema kunywa juisi baada ya chakula na siyo wakati wa chakula.

Pangilia vizuri chakula chako, epuka kula vyakula vya aina nyingi kwa wakati mmoja. Picha|Mtandao. 

Matunda na mboga za majani usizipe kisogo

Mboga za majani pekee zina vitamini na madini mengi kuliko chakula cha aina yoyote ile. Zina kosa vitamini D tu ambayo mwili huitengeneza kupitia nishati ya jua. 

Lakini kanuni hizo zitakuwa na ufanisi kama kutakuwa na muunganiko mzuri wa kupumzika kabla ya kula na kutembea kidogo baada ya kula. Siyo tofauti na huo.

Ni kanuni rahisi kukumbuka na kuzoeleka. Ukiamua kuzitumia, chakula peke yake na mtindo mzuri wa chakula na ulaji wako unakuweka katika sehemu nzuri ya kuwa na afya njema.   

Related Post