Zingatia haya kabla hujanunua bidhaa mtandaoni

November 14, 2019 12:56 am · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Jiridhishe na aina ya kampuni inyotoa huduma ya manunuzi mtandaoni kama ina uhalali.
  • Pitia sera za fidia na kurudisha bidhaa kama zina tija kwako. 
  • Hakiki anuani ya mahali unapoishi ili kuepuka mzigo kupotea.

Manunuzi ya bidhaa na huduma mtandaoni yanaongezeka kwa kasi duniani kutokana na ukuaji wa teknolojia na uhitaji wa watu kupata vitu kutoka sehemu tofauti duniani. 

Kabla ya kufanya manunuzi ya bidhaa mbalimbali mtandaoni, kuna baadhi ya vitu unavyotakiwa kuzingatia ili kupata bidhaa halisi uliyonunua na yenye kukidhi matakwa yako.

Izingatiwe kuwa bidhaa za mtandaoni huwezi kuzishika badala yake unaziona kwa picha na taarifa zake. Sasa zingatia haya wakati ukifanya manunuzi yako mtandaoni.

Jambo la kwanza kabla hujafanya manunuzi mtandaoni, jiridhishe na tovuti, programu tumishi au mahali unapofanyia manunuzi yako kama ni mfumo unaojulikana na unaweza kukupa bidhaa na huduma unayotaka.

Hii itakusaidia kuepuka matapeli ambao wanatumia mtandao kujipatia fedha kwa njia isiyo halali.

Baada ya kuhakikisha kama tovuti au programu tumishi ni sahihi kuna haja ya kuangalia kama programu tumishi hiyo inatoa huduma halisi. Mfano kama programu inawezesha kuuza nguo, iwe kweli inahusika na biashara hiyo.

Utambulisho wa programu tumishi ni muhimu kwa mteja kama anafanya malipo, kupata nakala ya risiti kuonyesha kwamba amefanya malipo ya kitu fulani kwa muda muafaka.


Zinazohusiana:


Mahali mzigo wako unatakiwa kufika ni jambo lingine la kuzingatia kwa sababu, wakati mwingine  bidhaa inaweza kwenda kwa mtu asiye sahihi na kusababisha upotevu wa mzigo.

Hakiki anuani ya mahali unapoishi ili mzigo ukufikie kwa wakati na kuepuka usumbufu usio wa lazima.

Kama mteja unatakiwa kujua sera ya fidia na kurudisha (Return & Refund policy) ya kampuni husika mtandaoni ili kukuweka katika nafasi nzuri ya kukwepa hasara ikiwa mzigo utapata changamoto. Fahamu vizuri taratibu za kurudisha mzigo kama haukidhi mahitakji yako.

Kitu cha mwisho cha kuzingatia ni kuangalia maoni ya watu waliyowahi kutumia huduma husika ya manunuzi mtandaoni. Maoni ya watu yatakupa picha kamili ya ufanisi na ubora wa mfumo unaotaka kutumia kwa manunuzi mtandaoni.

Hata hivyo, manunuzi ya bidhaa kwa njia ya mtandao ni njia rahisi ya kujipatia bidhaa popote ulipo kwa kutumia simu yako ya mkononi, jambo linalookoa muda na gharama za kwenda dukani moja kwa moja.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
13 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
13 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV