Ziara ya Rais Samia Ubelgiji yaleta neema Tanzania

March 11, 2022 5:36 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Emmanuel Tutuba, akizungumza wakati wa kikao na ujumbe kutoka Ubelgiji, jijini Dodoma. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Jestas Nyamanga, na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Khamis Shaaban. Picha| Wizara ya Fedha na Mipango.


  • Ubelgiji yaahidi kuipatia Tanzania Sh62 bilioni.
  • Zitatumika kukuza ujuzi wa ajira kwa vijana wa Kigoma.
  • Ziara ya Rais Samia yamia yachangia kupatikana kwa fedha hizo.

Dar es Salaam. Serikali ya Ubelgiji imeahidi kuipatia Tanzania Euro milioni 25 sawa na Sh62 bilioni, kwa ajili ya kutekeleza programu mpya ya maendeleo ya miaka mitano katika sekta ya elimu inakayosaidia kukuza ujuzi wa ajira kwa vijana.  

Programu hiyo inayotarajiwa kutekelezwa kuanzia mwaka 2023 hadi mwaka 2027 katika mkoa wa Kigoma.

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Ubelgiji (ENABE), Koenrad Goekint  ametoa ahadi hiyo Machi 10, 2022 baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Katibu MKuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Emmanuel Tutuba.

Goekint amesema kuwa programu hiyo itajikita katika kuendeleza sekta ya elimu kwa kuangazia maeneo ya ukuzaji ujuzi wa ajira na utaalam kwa vijana hususan masuala ya uanagezi na ujasiriamali.

Itasaidia kuzalisha ajira, kuimarisha usawa wa kijinsia kwa kukuza zaidi ushiriki wa wanawake kwenye shughuli za maendeleo na kuboresha masuala ya usawa wa kijinsia nchini.

Tutuba ameishukuru ENABEL kwa kuja na program hiyo itakayotoa matokeo mazuri kwa kugusa maisha ya wananchi wa Tanzania katika kuwaletea maendeleo.

“Program hii itakayotekelezwa mkoani Kigoma itagusa maeneo ya kipaumbele yaliyoainishwa kwenye utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2021/22 – 2025/26), wenye lengo la kuboresha huduma za jamii, maisha ya watu na elimu ni moja ya maeneo hayo” amesema Tutuba.


Soma zaidi:


Tutuba ameiomba Serikali ya Ubelgiji kuangalia uwezekano wa kuongeza maeneo mengine ya kimkakati ya kuboresha maisha ya wananchi ikiwemo huduma za afya na maji kwani wanawake ndiyo walengwa wakuu na ndiyo wanaokabiliana na changamoto ya uhaba wa maji.

Ameshauri Serikali ya Ubelgiji kutekeleza mradi kama huo kwa upande wa Zanzibar ili kuwawezesha wananchi wa visiwa hivyo kufurahia matunda mazuri ya uhusiano mwema uliopo kati ya Tanzania na Ubelgiji.

Utoaji wa fedha hizo ni matokeo ya ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyofanya kati ya Februari 14 na 19, 2022

Akiwa nchini Ubelgiji, Rais alikutana kwa mazungumzo na viongozi mbalimbali akiwemo Alexander De Croo, Waziri Mkuu wa Ubelgiji ambapo Viongozi hao walikubaliana kuweka mikakati ya kufanyika kwa majadiliano ya programu ya maendeleo na kuhakikisha kuwa mchakato wa maandalizi unakamilishwa kwa wakati.

Tanzania imeingia katika orodha ya nchi 15 pekee duniani ambazo Ubelgiji  inaendesha programu kama hiyo, jambo ambalo ni ishara ya mafanikio makubwa ya uhusiano uliopo kati ya nchi hizi mbili.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV