Rais Samia adokeza vipaumbele Dira ya Maendeleo 2050

December 9, 2023 1:18 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni pamoja na kuchochea ukuaji wa uchumi ili kuongeza upatikanaji wa ajira kwa wananchi.

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imebainisha baadhi ya maeneo yatakayopewa kipaumbele katika maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050 ikiwemo kuchochea ukuaji wa uchumi kwenye maeneo ya uzalishaji yanayowagusa wananchi.

Rais Samia Suluhu Hassan, amewaeleza washiriki wa hafla ya maadhimisho ya miaka 62 ya uhuru wa Tanzania Bara jijini Dodoma leo Disemba 9, 2023, vipaumbele hivyo vimetokana  na ripoti ya tathmini ya utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025 itakayomalizika miaka miwili ijayo. 

“Maeneo yatakayopewa kipaumbele ni kama ifuatavyo ukuaji wa uchumi kufugamanishwa na sekta za uzalishaji kama kilimo na nyingine za uzalishaji,” amesema Rais Samia.

Amesema dira hiyo iwe na kipaumbele cha kuchochea ukuaji wa uchumi katika maeneo ya uzalishaji yanayomgusa mwananchi mmoja mmoja, jambo litakalochochea upatikanaji wa ajira.

Baadhi ya wahudhuriaji wa maadhimisho ya miaka 62 ya uhuru wa Tanzania Bara na Mkutano wa Kwanza wa Kitaifa wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.Picha|Ikulu

Kitabu cha hali ya uchumi kwa mwaka 2022 kilichotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kinabainisha kuwa hadi kufikia mwaka 2020/2021 Tanzania ilikuwa na asilimia 12.9 ya vijana wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 35 wasiokuwa na ajira. Hii ina maana kuwa vijana 13 kati ya 100 wenye umri huo hawakuwa na ajira inayowasaidia kuingiza kipato. 

Vijana wenye umri wa miaka 15 mpaka 35, kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi kwa mwaka 2022, walikuwa milioni 20.6.  Kwa idadi hiyo, ina maana kuwa zaidi ya vijana milioni 2.6 wenye umri wa miaka 15 hadi 35 hawana ajira nchini ukiachana na wale wenye umri huo ambao bado wapo masomoni.

Rais Samia amebainisha pia kuwa dira mpya ya mwaka 2050  itaimarisha uendeshaji wa mashirika ya Serikali pamoja na yale sekta binafsi kutoka ndani na nje ya nchi huku ikifanya tathmini na ufuatiliaji katika utekelezaji wa mipango yote ya nchi.

Kipaumbele cha tathmini na ufuatiliaji wa mipango ya nchi kimewekwa chini ya tume ya mipango ambayo muswada wake umeidhinishwa  na Bunge hivi karibuni. Tume hiyo inatarajiwa kusaidia utekelezaji wa shughuli nyingine za maendeleo nchini.

“Uwepo wa taasisi ya tume ya mipango utakwenda kuondosha changamoto hiyo…si katika utekelezaji wa dira ijayo tu bali katika utekelezaji wa mipango yote ya maendeleo ya nchi yetu,” amesema Rais Samia.


Soma zaidi:Jinsi Tanzania inavyoweza kuongeza upatikanaji wa haki za binadamu


Serikali pia kupitia dira ya mwaka 2050 ina mpango wa kuyaimarisha mashirika ya umma na sekta binafsi  ili ziweze kujiendesha kwa faida na kukuza uchumi wa taifa 

“Dira iweke uelekeo wa uwekezaji na usimamizi wa maboresho ya kiutendaji wa mashirika ya Serikali ili yaongeze ufanisi katika uendeshaji na yaweze kuhimili ushindani wa kikanda na kimataifa…sekta binafsi Serikali tupo tayari kuwaimarisha na muwe tayari kuimarika,” amesema Rais Samia.

Itakumbukwa kuwa Agosti 19, 2023 jijini Arusha, Rais Samia aliyataka  mashirika  ya umma kujitegemea na kujiendesha  kwa faida ili kupunguza mzigo kwa Serikali.

Pia alitoa mapendekezo ya kuanzishwa kwa mifuko utakaosimsmia mashirika hayo ili  kuondoa utegemezi kutoka mfuko mkuu wa Serikali.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV