Wizara ya Habari yaomba kuidhinishiwa bajeti ya Sh525.32 bilioni mwaka wa fedha 2026/27

May 4, 2026 3:27 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Bajeti yaongezeka kwa asilimia 1.1 kutoka mwaka 2025/26.
  • Zaidi ya Sh458 bilioni kuelekezwa kwenye miradi ya maendeleo na maandalizi ya matukio makubwa ya kimataifa.

Dar es Salaam .Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeomba Bunge kuidhinisha bajeti ya jumla ya Sh525.32 bilioni  kwa mwaka wa fedha 2026/27 kwa ajili ya kutekeleza majukumu na vipaumbele vya wizara hiyo.

Waziri Paul Makonda aliyekuwa akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo leo Mei 4,2026  bungeni jijini Dodoma, amesema kati ya fedha zinazoombwa, Sh39.71 bilioni  zimetengwa kwa ajili ya mishahara.

“Sh28.65 bilioni matumizi mengineyo na miradi ya maendeleo Sh 458.19 milioni,” amesema Makonda.

Bajeti ya mwaka 2026/27 imeongezeka kwa Sh5.66 bilioni sawa na asilimia 1.1 kulinganisha na ile ya mwaka unaoishia Juni 20,2026.

Katika mwaka wa fedha 2025/26, Wizara iliidhinishiwa Sh519.66 bilioni, ambapo Sh33.41bilioni zilikuwa kwa ajili ya mishahara, shilingi bilioni 28.07 matumizi mengineyo, na shilingi bilioni 458.19 kwa miradi ya maendeleo.

Waziri huyo ameeleza kuwa katika mwaka 2026/27, Wizara imejipanga kutekeleza maeneo mbalimbali ya kimkakati yatakayochochea maendeleo ya sekta za habari, utamaduni, sanaa na michezo nchini.

Vipaumbele vya wizara 

Miongoni mwa maeneo ya kipaumbele ni kukamilisha ukarabati, ujenzi, uboreshaji na utunzaji wa miundombinu ya sekta hizo, pamoja na kukamilisha maandalizi ya Tanzania kuwa mwenyeji wa Mashindano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027 yatakayofanyika kuanzia Juni hadi Julai 2027.

Aidha, Wizara imepanga kuhakikisha Tanzania inakuwa mwenyeji wa Mashindano ya 74 ya Urembo ya Dunia (Miss World), sambamba na kuendelea kuhuisha sera, sheria, mikakati, miongozo na kanuni mbalimbali kwa lengo la kuimarisha usimamizi na utekelezaji wa shughuli za sekta husika.

Vipaumbele vingine ni pamoja na kuimarisha matumizi ya Kiswahili katika ngazi ya kikanda na kimataifa, kuwezesha ushiriki wa timu za taifa katika mashindano ya kimataifa, kuboresha elimu na mafunzo katika tasnia za utamaduni, sanaa na michezo, pamoja na kuimarisha mazingira wezeshi kwa sekta binafsi kushiriki katika kukuza sekta hizo.

Wizara pia imejipanga kuratibu na kusimamia matamasha, shughuli na matukio makubwa ya kitaifa na kimataifa yanayohusiana na habari, utamaduni, sanaa na michezo.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
20 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
20 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
20 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Nukta TV

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

Nukta TV

Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Nukta TV