Wizara ya Afya: Hakuna wagonjwa wengi wa Corona Hospitali ya Rufaa Shinyanga

July 11, 2021 12:17 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Imesema taarifa zinazosambazwa ni za uongo.
  • Yakanusha mitungi ya oksijeni kutokukidhi mahitaji ya wagonjwa.

Dar es Salaam. Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema taarifa zinasambaa mtandaoni kuwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga imeelemewa na wagonjwa wa COVID-19 siyo za kweli.

Licha ya kutokuwepo kwa wagonjwa wengi, Imesema imejiridhisha kuwa siyo kweli mitungi ya oksijeni haikidhi mahitaji wa wagonjwa wa COVID-19 hospitalini hapo.

“Hii taarifa ni ya uzushi,” imesema Wizara ya Afya katika ukurasa wake wa Twitter leo Julai 11, 2021 ikitolea maelezo moja ya taarifa inayodaiwa kuwa ni ya upotoshaji katika mtandao huo.

Taarifa hiyo ya wizara imekuja baada ya kusambaa kwa taarifa hasa katika mtandao wa Twitter kuwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga inakabiliwa na wagonjwa wengi wa COVID-19, jambo linalosababisha mitungi ya oksijeni kuwa michache.Kujilinda na habari za uzushi, wananchi wanashauriwa kupata taarifa za Corona kutoka mamlaka za afya ikiwemo Wizara ya Afya na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Hata hivyo, Serikali ya Tanzania imeendelea kuwasisitiza wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo kwa kunawa mikono, kuvaa barakoa na kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV