Without Remorse: Safari ya kisasi inavyobadili maisha ya afisa wa jeshi
- Inamhusu mwanajeshi anayepambana kulipa kisasi baada ya kifo cha mke wake.
- Inagundulika kuwa aliyemuuza yeye na wenzie ni afisa wa jeshi anayepigania maslahi ya nchi yake.
- Anapomuua muuwaji wake, anarudi kumtafuta afisa huyo anayeonja joto ya jiwe.
Dar es Salaam. Kila mtu ana kitu ambacho kikiguswa na adui basi huo ndio mwisho wa hasimu wake. Kwa wengine ni mali zao, kwa wengine ni kazi na kwa wengine ni familia yaani mtoto, mama, baba na mke.
Na hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa mwanajeshi John Kelly ambaye kifo cha mkewe bi Pam kiliwafanya walioshiriki kuonja joto ya jiwe. Fahamu zaidi kwa kutazama filamu ya “Without Remorse”
John Kelly ni chifu wa jeshi la majini na kwa sasa furaha yake ipo kwa mke wake Pam ambaye anatarajia kujifungua mtoto wao wa kwanza siku chache zijazo. Kama baba mtarajiwa, Kelly amejaa tabasamu na kila akimuona mkewe Pam, ni kama anaapa kufanya kila linalowezekana kumlinda, kumpenda na kumthamini.
Hata hivyo, wakati akihisi yupo kwenye usalama, mashua ya familia yake inaharibika na kutia nanga nchi kavu. Historia inaanza kumtafuna yeye na familia yake.
Miezi kadhaa iliyopita, Kelly alikuwa miongoni mwa kikosi cha kumkomboa mpelelezi wa CIA ambaye alikuwa alishikiliwa mateka nchini Syria. Baada ya kumkomboa, huenda yeye na wenzie walifanya sherehe ya kujipongeza bila kujua kuwa historia hiyo ingelianza kuwatafuna mmoja baada ya mwingine.
Siku hiyo, ghafla taa za nyumbani kwake zilizimwa na watu wasiojulikana na kama baba wa familia, taratibu anatafuta silaha yake ilipo ili atetee ngome yake. Hata hivyo juhudi zake zinafua dafu kwa kuwaua majambazi wote kasoro mmoja ambaye anafanikiwa kumwacha Kelly na risasi mwilini mwake na fahamu zikimpotea.
Bahati mbaya zaidi, ni kuwa katika mapambano hayo, mke mjamzito wa Kelly anauwawa na hapo ndipo mwaka huo unakuwa wa kusimuliwa kwa wote waliohusika.
Wakati akihisi yupo kwenye usalama, mashua ya familia yake inaharibika na kutia nanga nchi kavu. Picha| Slash Film.
Pale Kelly anapofunbua macho baada ya kupona, inagundulika kuwa waliohusika katika shambulio lake ni Warusi.
Anamtafuta mwanadiplomasia wa Kirusi ambaye anampatia jina la muuaji ambaye amebaki na kujua ni nani yupo nyuma ya kufichua majina ya waliofanya uokozi wa mwana CIA ambao uliofanywa kwa siri kiasi cha wengi kutokujua waliohusika katika uokozi.
Mtu mahali anasema yasiyopaswa kwa wasiopaswa.
Safari ya kumtafuta gaidi Victor Rykov inaanza ikimuhusisha Kelly na wanajeshi wengine wa CIA ambapo kumfikia Rykov, inabainika kuwa ulikuwa ni mtego wa kuwamaliza wapambanaji hao wote baada ya Rykov kujilipua. Ni harufu ya kuwa mtu mmoja mahala anavujisha siri na mipango ya CIA.
Soma zaidi:
- Umafia na wema: Filamu ya “Raya and the Last Dragon” inavyofundisha ujasiri, umoja
- Guterres: Muziki wa Jazz ni alama ya uhuru, utu
- Maumivu: Bei ya petroli, dizeli yapanda miezi mitatu mfululizo
Kelly anamhisi mwenzake anayejulikana kwa jina la Ritter kuwa huenda yeye ndiye anayevujisha siri za jeshi lakini Ritter anakataa kuwa siye na hisia zake zinampotosha.
Wakati Rykov anajilipua, timu hiyo pia inanza kushambuliwa na risasi za majasusi ambapo Kelly anaamua kubaki kama mbuzi wa kafara ili wenzake wajiokoe.
Licha ya kuwa amaumia, anafanikiwa kutoka akiwa salama na Ritter anamsaidia kuigiza kifo chake ili asirudi kutumikia kifungo cha kumuua mwanadiplomasia wa Kirusi.
Baada ya yote hayo, Katibu wa ulinzi, Thomas Clay anajitokeza na kusema kuwa yeye ndiye amekuwa akipanga mambo hayo yote ili kuanzisha vuguvugu la vita baridi kati ya Marekani na Warusi na ni njia aliyokuwa akiitumia kuwaunganisha Wamarekani. Anakuwa amejikaanga mwenyewe.
Siku inakuja ambapo Kelly analazimika kutengeneza kifo cha Katibu Clay na baada ya kufanikiwa, Kelly anajipatia utambulisho mpya ambapo anaishi kwa furaha kama John Clark japo bila mke na mtoto.
Latest