WHO yasikitishwa kasi ndogo ya utoaji chanjo ya Uviko-19 Afrika

August 26, 2021 6:59 am · Medlini
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni nchi nne zimeweza kufikia kiwango cha  asilimia 10 ya wananchi wake wote kupata chanjo.
  • Afrika imepata chonjo milioni 87 mpaka sasa
  • Ukosefu wa chanjo na utayari wachangia kazi ndogo ya utoaji chanjo.

Dar es Salaam. Huenda ikachukua muda kwa nchi za Afrika kupunguza kasi ya maambukizi ya Corona (Uviko-19) kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo mwenendo usiorodhisha wa utoaji wa chanjo dhidi ya ugonjwa huo unaoutesa dunia kwa sasa.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa mataifa la Afya UlimwenguNI (WHO) Dk Tedros Ghebreyesus amesema ni nchi nne tu za Afrika ambazo zimeweza kufikia kiwango cha  asilimia 10 ya wananchi wake wote kupata chanjo.

“Ulimwenguni, nchi 140 angalau zimechanja wananchi wake kwa asilimia 10, lakini kati ya nchi hizo za kutoka Afrika ni nchi 4 pekee ndio zimeweza kufikia kiwango hicho cha asilimia 10 ya wananchi wake wote, na utofauti huu ni kutokana na kukosa chanjo,” amesema Ghebreyesus.

Dk Ghebreyesus ametoa masikitiko hayo katika mkutano wa kamati ya mawaziri wa afya barani Afrika unaofanyika kwa siku tatu nchini Togo.

Aidha, amesema kuwa usambazaji wa chanjo umekuwa si wa haki kwa kiasi kikubwa kwa sababu ulimwenguni kote chanjo zilizotolewa ni zaidi ya bilioni 4.8 huku Afrika akipata chanjo milioni 87 tu kati ya hizo. 

Kiwango hicho cha chanjo ya Uviko-19 kilichofika Afrika ni chini ya asilimia mbili huku akizitaka Serikali na wataalam wa afya kulitazama suala hilo kwa makini ili kuokoa maisha ya watu.

“Hivyo tunatarajia kuona ongezeko la kasi ya utoaji chanjo, mwezi Julai chanjo zimesambazwa kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na miezi mitano iliyopita, malengo yetu ni kufikia chanjo milioni 475 ifikapo mwezi Disemba mwaka huu 2021,” Amesema Dk Ghebreyesus.

Pia mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika Dk Matshidiso Moet amesema sektretarieti yake imejipanga vyema kwa miaka ijayo na  wanategemea kuimarisha namna ya kukabiliana na Uviko-19 hususan kwenye chanjo ambayo ndiyo itakuwa sehemu muhimu ya kazi yao lakini hii itaenda pamoja na kuimarisha mifumo ya afya.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV