Waziri Kigwangalla: Kazi ya kuzima moto uliozuka Mlima Kilimanjaro ni ngumu

October 15, 2020 5:57 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Amesema kazi ya kuzima moto uliozuka mwishoni mwa wiki ni ngumu na kubwa kuliko inavyodhaniwa.
  • Ugumu huo unasababishwa na upepo mkali na kukauka kwa nyasi na vichaka. 
  • Helikopta na ndege kuanza kutumika kuzima moto huo ikiwa taratibu zitakamilika leo.

Dar es Salaam. Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla amesema kazi ya kuzima moto uliozuka Mlima Kilimanjaro mwishoni mwa wiki ni ngumu na kubwa kuliko inavyodhaniwa kwa sababu ya changamoto ya upepo mkali na kukauka kwa nyasi na vichaka. 

Moto huo ulizuka Jumapili Oktoba 11, 2020 katika eneo la Whona ambacho ni kituo cha kupumzikia wageni wanaotumia njia ya Mandara na Horombo kupanda mlima huo mrefu kuliko yote Afrika.

“Bado tunahangaika na kuzima moto. Kazi ni ngumu na kubwa kuliko inavyodhaniwa. Changamoto ni upepo mkali na kukauka kwa nyasi na vichaka,” ameandika Dk Kigwangalla katika ukurasa wake wa Twitter leo (Oktoba 15, 2020).

Amesema kutokana na hali hiyo, wanakusudia kutumia helikopta na ndege kudhibiti moto huo.

“Taratibu zikikamilika leo tutaweza kuanza kutumia helikopta na ndege kuzima moto,” amesema Waziri huyo.

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Mawasiliano wa Tanapa, Pascal Shelutete katika taarifa yake iliyotolewa Oktoba 13, 2020 alisema kazi ya  helikopta hiyo itakuwa ni kuangalia eneo lililoathirika na kufuatilia maeneo mengine yanayoweza kushika moto.

Amesema jumla ya nguvukazi ya watu 500 wako eneo la tukio kukabiliana na moto huo ambao kwa sehemu kubwa tayari umedhibitiwa. 


Soma zaidi:


Hata hivyo, Tanapa imesema inachukua tahadhari zote ili kuhakikisha usalama wa wageni na vifaa vyao unaimarika bila kuathiri shughuli za utalii ambazo zinaendelea kama kawaida hususan njia ya Marangu iliyoathirika na moto husika.

Mamlaka zinaeleza kuwa wastani wa watu 50,000 hupanda mlima huo kila mwaka.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
16 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
17 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
17 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Nukta TV

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Nukta TV

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV